Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa habari, Mawasiliano na Uhusiano Serikalini (TAGCO), Pascal Shelutete(katikati) akiongea na waandishi wa habari kuhusu kikao kazi cha chama hicho kinachotarajiwa kufanyika Machi mwaka huu Jijini Mbeya, kulia ni Mhariri Mkuu kutoka Idara ya Habari –MAELEZO, Elius Malima na kushoto ni Katibu Mwenezi TAGCO, Dkt. Cosmas Mwaisoba.
Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa habari, Mawasiliano na Uhusiano Serikalini (TAGCO), Pascal Shelutete(kulia) akiongea na waandishi wa habari kuhusu kikao kazi cha chama hicho kinachotarajiwa kufanyika Machi mwaka huu Jijini Mbeya, kushoto ni Katibu Mwenezi TAGCO, Dkt. Cosmas Mwaisoba.
……………..
Na. Paschal Dotto-MAELEZO
Kikao kazi cha Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano Serikalini (TAGCO) kinatarajia kufanyika Machi 9-13, 2020 Jijini Mbeya ambapo Zaidi ya Maafisa 400 wanatarajia kuhudhuria Mkutano huo ambao utaangazia Zaidi katika kuangalia nini sekta hiyo muhimu imetekeleza katika azma ya kuisemea serikali kwenye kazi inazotekeleza kwa wananchi.
Akizungumza katika Mkutano na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa TAGCO Pascal Shelutete alisema kuwa kikao hicho kitalenga kuimarishha kada hiyo kwenye Taasisi za Serikali ili kuweza kutangaza mambo yanayofanywa na Serikali kwa wananachi.
“Kikao kazi hiki ni mwendelezo wa vikao vinayofanyika kila mwaka kwa lengo la kuwajengea
Washiriki uwezo na pia kuimarisha Idara/Vitengo vya Mawasiliano na Uhusiano Serikalini
katika kutangaza shughuli za Serikali hasa mafanikio katika utendaji wa Serikali ya Awamu ya Tano” alisema Shelutete.
Kikao hicho kinaratibiwa na Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) kwa kushirikiana na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kinafanyika kwa mara ya 15 ambapo mwaka jana kilifanyika Machi 18 Jijini Mwanza.
Kikao hicho kitahusisha Maafisa Habari, Mawasiliano, Uhusiano na Itifaki wa Wizara, Idara zinazojitegemea, Taasisi, na Wakala wa Serikali (MDAs), pamoja na kutoka katika Mikoa na Halmashauri mbalimbali ambapo washiriki watafanya tathmini ya utendaji kazi wao kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita.
TAGCO ilianzishwa rasmi mwaka 2012 na kusajiliwa kwa mujibu wa sheria za
Nchi, na inajumuisha watumishi wa umma wanaoshughulika na masuala ya habari,mawasiliano, uhusiano na itifaki Serikalini.