Home Michezo SAMATTA AANZA NA NEEMA ASTON VILLA

SAMATTA AANZA NA NEEMA ASTON VILLA

0

DOUGLAS Luiz, nyota wa Aston Villa alirejesha nguvu kwenye timu yake dakika ya 68 baada ya kufunga bao kali la kusawazisha bao la wapinzani wao Watford kwenye mchezo wa Ligi Kuu England.

Bao la kuongoza kwa Watford lilifungwa na Troy Deeney dakika ya 38 ya kipindi cha kwanza na liliwapeleka mapumziko wakiwa mbele kwa bao hilo ambalo lilisawazishwa kipindi cha pili.

Bao la ushindi wakati Aston Villa ambayo ni timu mpya ya Mtanzania, Mbwana Samatta lilipachikwa dakika ya 90+5 na Tyrone Mings na kuifanya timu hiyo ishinde kwa mabao 2-1.

Ushindi huo unaifanya Aston Villa kufikisha jumla ya pointi 25 ikiwa nafasi ya 16 kwenye msimamo wa Ligi na Watford kuwa nafasi ya 19 na pointi zao 23 na wote wamecheza mechi 24 hivyo kufanya Samatta kuanza kwa neema 

Mchezo wao unaofuata wa Ligi utakuwa Februari, Mosi dhidi ya Bournermouth ugenini na Samatta anatarajiwa kuanza kuonyesha makeke.