Home Mchanganyiko WAZIRI KAIRUKI ATEMBELEA KIWANDA CHA KUBANGUA KOROSHO CHA SABAI MKURANGA

WAZIRI KAIRUKI ATEMBELEA KIWANDA CHA KUBANGUA KOROSHO CHA SABAI MKURANGA

0

Meneja wa kiwanda cha kubangua korosho cha SABAI Bw. Yonathan Kamee akimuonesha Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki mashine ya kubangulia korosho alipotembelea kiwanda hicho kilichopo katika Kata ya Kiparang’anda Wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani ili kuona uwekezaji huo, Januari 20, 2020

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki akiangalia korosho zilizobanguliwa na mashine maalum katika kiwanda cha kubangua, kukausha na kudarajisha korosho cha SABAI Kilichopo Kata ya Kiparang’anda Wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani Januari 20, 2020.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki akieleza namna Serikali inavyoendelea kuboresha mazingira ya wawekezaji nchini kwa uongozi wa kiwanda cha kubangua na kukausha korosho cha SABAI. Bw. Daniel Marwa (mwenye miwani) ni mmiliki wa kiwanda hicho.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Bw. Filberto Sanga wakati wa ziara yake ya kikazi katika kiwanda cha Kubangua na kukausha korosho cha SABAI Mkuranga Pwani, Januari 20, 2020.

Mmiliki wa kiwanda cha kubangua na kukausha korosho cha SABAI Bw. Daniel Marwa kimuonesha Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki korosho iliyobanguliwa na kiwanda hicho, alipotembelea kiwandani hapo Januari 20, 2020.

Meneja wa kiwanda cha kubangua na kukausha korosho cha SABAI Bw. Yonathan Kamee akimuonesha Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki mazingira ya kiwanda hicho wakati wa ziara yake ya kikazi kiwandani hapo.