Home Mchanganyiko SHONZA AONGOZA WAJUMBE WA UMOJA WA POSTA AFRIKA KUTEMBELEA HIFADHI YA TARANGIRE

SHONZA AONGOZA WAJUMBE WA UMOJA WA POSTA AFRIKA KUTEMBELEA HIFADHI YA TARANGIRE

0
Naibu Waziri Wizara ya Habari,Utamaduni ,Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza (kushoto)akiongozana na Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Tarangire Neema Mollel kuwaongoza wajumbe wa Umoja wa Posta Afrika, waliyotembelea hifadhi hiyo kuelekea eneo la mto Tarangire eneo la Matete Picnic Site Januari 19 Jijini Arusha.
Naibu Waziri Wizara ya Habari,Utamaduni ,Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza (kushoto)na wajumbe wa Umoja wa Posta Afrika wakimsikiliza Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Tarangire Neema Mollel (kulia) akitoa maelezo kuhusu Mto Tarangire na sifa za mto huo wakati wajumbe hao walipotembelea Matete Picnic Site Januari 19 jijini Arusha.
Naibu Waziri Wizara ya Habari,Utamaduni ,Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza akifurahia jambo na Kaimu Katibu Mtendaji Mamlaka ya Tume ya Usimamizi wa Huduma za Posta kutoka nchini Ghana Bibi.Hamdaratu Zakaria alipokuwa akizungumza kuhusu ukarimu na upendo wa watanzania, wakiti wakiwa ndani ya hifadhi ya Tarangire iliyopo jijini Arusha iliyotembelewa na wajumbe wa Umoja wa Posta Afrika .
Naibu Waziri Wizara ya Habari,Utamaduni ,Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza (kulia) akimuhoji swali Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Tarangire Neema Mollel (kushoto) kuhusu fuvu la kichwa cha tembo lililowekwa kwa ajili ya maonesho ya kuonyesha namna hifadhi hiyo inatembo wengi wakati wa ziara ya wajumbe wa Umoja wa Posta Afrika katika hifadhi hiyo Januari 19 jijini Arusha.
Naibu Waziri Wizara ya Habari,Utamaduni ,Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani ndani ya hifadhi ya Tarangire mara baada ya kumalizika kwa ziara ya kuwatembeza wajumbe wa Umoja wa Posta Afrika katika hifadhi hiyo Januari 19 jijini Arusha ambapo amewasihi kuwa mabalozi wazuri wa kutangaza hifadhi hiyo Afrika.

…………………………………………………………….

Na Anitha Jonas – WHUSM – Tarangire

Naibu  Waziri Wizara ya Habari,Utamaduni ,Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza awasihi wajumbe wa Umoja wa Posta Afrika (PAPU) kuwa Mabalozi wazuri wa kuitangaza hifadhi ya Tarangire.

Mhe.Shonza amteoa kauli hiyo hivi karibuni jijini Arusha alipokuwa akifanya ziara ya kuwaongoza wajumbe wa Mkutano wa Maadhimisho ya Miaka 40 ya PAPU yaliyofanyika hivi karibuni jijini Arusha  kutembelea hifadhi hiyo .

“Naamini mmefurahia kutembelea hifadhi hii,na Tanzania imebarikiwa kuwa na hifadhi nyingi ikiwemo Serengeti,Ngorongoro,Manyara na nyingine nyingi ombi langu kwenu ni mkawe mabalozi wazuri katika nchi zenu kutangaza fursa hii ya utalii yaw a hifadhi ya wanyamapori,”alisema Mhe.Shonza.

Akiendelea kuzungumza baada ya  kukamilika kwa ziara hiyo ya kutembelea hifadhi hiyo Naibu Waziri huyo alitoa wito kwa wadau mbalimbali kutoka nchi za Afrika kuja kuwekeza nchini kwani kuna usalama na amani, pia alitoa pongezi kwa uongozi wa  PAPU kwa maadhimisho ya miaka 40 na hatua ya ujenzi wa ofisi yao ya Makao Makuu jijini hapo.

Naye Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Tarangire Neema Mollel aliushukuru uongozi wa sekta ya Mawasiliano uliyoandaa mkutano huo kwa kuichagua hifadhi hiyo kutembelewa na wageni hao kutoka nchi mbalimbali kwani anaamini wageni hao watasaidia kuwa mabalozi wa kutangaza hifadhi hiyo yenye utajiri wa miti mingi ya mibuyu na wanyama mbalimbali wakiwemo,Simba,Tembo,Twiga , Ngiri,Swala na mto wenye viboko wengi ambapo samba hutumia eneo hilo kuwinda nyumbu wanapokwenda kunywa maji.

Pamoja na hayo nae Katibu Mtendaji  Mamlaka ya Tume ya Usimamizi wa Huduma za Posta kutoka nchini Ghana Bibi.Hamdaratu Zakaria alishukuru viongozi wa Tanzania kwa kuwapa fursa  ya kutembelea hifadhi hiyo kwani amefurahia sana kuona wanyama mbalimbali akiwemo Twiga,Tembo, Swala,Mbuni na Ngiri,pia alisema amefurahishwa na utamaduni wa ukarimu kutoka kwa watanzania pamoja hali ya usalama na amani iliyopo.