Home Burudani Ngoma Africa Band Kutumbuiza Black History Month Jijini Hamburg,Ujerumani  Jumamosi 1 February...

Ngoma Africa Band Kutumbuiza Black History Month Jijini Hamburg,Ujerumani  Jumamosi 1 February 2020

0
Bendi maarufu ya Muziki wa dansi barani ulaya The Ngoma Africa Band aka FFU-Ughaibuni ukipenda waite viumbe wa ajabu Anunnaki au “Watoto wa Mbwa” inayoongozwa na kamanda Ras Makunja inatarajiwa kulitingisha jukwaa la  Black History Month katika ya jiji la Hamburg katika ukumbi wa Gruenspan Ujerumani siku ijumaa tarehe 1-02-2020 kuanzia majira ya saa 2.00 usiku (20.00 hour),bendi hiyo maarufu inayodumu kwa miaka 27 katika majukwaa ya kimataifa na mtindo wake wa “Bongo Dansi” made in Uswahilini inazidi kuwanasa washabiki katika kila pembe barani ulaya,ni juzi kati tu wameachia CD yao mpya  “Awamu Ya Tano Uwanjani” pia unaweza jumuika nao at www.facebook.com/ngomaafricaband au www.istagram.com/ngomaafricaband