Home Siasa SIASA ZA UBAGUZI ZANZIBAR ZAKEMEWA

SIASA ZA UBAGUZI ZANZIBAR ZAKEMEWA

0

********************************

Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni amesema ndani ya Chama cha Mapinduzi wezi hawavumiliwi huku akiwaasa wananchi wa Visiwa hivyo  kujikita kwenye shughuli za maendeleo na kujiepusha na siasa za ubaguzi zinazoweza kupelekea machafuko.

Masauni ameyasema hayo wakati wa kikao cha ndani na wanachama na wapenzi wa chama hicho kilichofanyika katika Ofisi za chama hicho Tawi la Mwembeladu na kufuatiwa na zoezi la usimikaji wa bendera katika makazi ya mabalozi ishirini lengo ni kuwaamsha wanachama kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.