Home Siasa NUKUU ZA DKT. BASHIRU ALLY KATIBU MKUU WA CHAMA CHA MAPINDUZI AKIZUNGUMZA...

NUKUU ZA DKT. BASHIRU ALLY KATIBU MKUU WA CHAMA CHA MAPINDUZI AKIZUNGUMZA NA MABALOZI, VIONGOZI WA MATAWI NA KATA WILAYA YA KOROGWE

0

******************************

14 Januari, 2020

1. “Hongereni sana kwa ushindi mnono wanaCCM uchaguzi wa serikali za mitaa kwa ushindi wa 100% na hapa Korogwe kwa historia, hili sio jambo jipya 2014 Korogwe mlipata 100% hivyo wale walioingia mitini kwa sababu walizozitaja ni uongo mtupu, kilichowapa mwaka jana, kiliwapatata 2014 hapa Korogwe, hata Monduli 2014 CCM ilishinda kwa 100%, asilimia mia kwa CCM katika uchaguzi wa serikali za mitaa si jambo jipya, jambo jipya ni wao kujitoa ili wasipate aibu.“

2. “Mbinu zile zile, ubunifu ule ule, mikakati ile ile ya 2019, 2020 wapate kipigo kile kile, na mwaka huu hakutakuwa na huruma, atakayeingia kugombea udiwani, ubunge, uwakilishi, Urais wa Muungano halali yetu, na kwenye Urais Zanzibar naye ni halali yetu, hiyo nayo ni demokrasia kwa kuwa kushindwa nayo ni demokrasia.”

3. “Leo natamka rasmi kuwa, mitambo ya ushindi nimeifunga rasmi mkoa wa Tanga, na kuna watu wanajiuliza kwa nini nimechelewa kuifunga , niwaeleze kuwa, sayansi ya kufunga mitambo ya Tanga ni lazima uanzie Unguja na Pemba, na huko tayari nilisha funga na makao makuu ya mitambo hiyo kwa Unguja ni Mkoa wa Mjini, kwa Pemba ni Mkoa wa Kaskazini,”

4. “Wao wakisikia CCM inafunga mitambo wanakimbilia kusema uchaguzi ni namba, leo ninawaeleza uchaguzi sio namba, wala tatu mzuka ambayo unacheza leo elfu moja kesho unapata milioni kumi, kushinda uchaguzi ni lazima uwekeze, uchaguzi ni uamuzi wa wananchi kuhusu hatma yao, hupati namba kama huna wanachama, mtandao wa wanachama , uwezo wa kuteua wagombea wenye sifa,, hupati namba kama huaminiki, hivyo uchaguzi sio namba, uchaguzi ni uamuzi wa umma kujua nani anasifa ya kuongoza , chama gani kinauwezo wa kusimamia maslahi ya wananchi, na Chama hiko kwa sasa ni CCM pekee.”

5. “CCM inauzoefu wa mapambano ya ukombozi wa Taifa hili, kina uzoefu wa uongozi, kilishapimwa, kikiahidi kinatenda, lakini Chama hiki kina hazina ya viongozi wenye hekima, bidii na wachapa kazi, hivyo CCM ni kiwanda cha kuzalisha viongozi bora ndani ya Chama chenyewe na ndani ya serikali..”

6. “Wananchi hawataki vyama vya uchaguzi, wanataka vyama vya uongozi, siku CCM ikishindwa kutekeleza majukumu yake wananchi wapate mbadala wa CCM, na Chama kitakacho hakiikisha umoja wa kitaifa unalindwa, uhakika juu ya ulinzi wa Mapinduzi yetu, kwa sasa Chama hiko hakipo, ila ruksa kwa watanzania wenye nia nzuri anzisheni vyama vyenu viwe na mwelekeo mzuri tofauti na vyama vya upinzani vya sasa ambavyo vyote vimechoka na vitakufa kimoja baada ya kingine.”

7. “Kwenye uchaguzi huwa kuna tabia ya wanaCCM wakishindwa kwenye uchaguzi wanahama Chama, leo niwaeleze, kuhama Chama ni haki ya kila mtu, ila ujue tu chama chochote utakachokwenda utafuatwa huko huko na kula kichapo, na msimu huu hakutakuwa na mchezo wa nyumbani kumenoga hata kama kumenoga utakaa huko huko na tutakuchapia huko huko, hivyo kamati za siasa mjipange kuwapa nasaha na ushauri wale wote wakaoshindwa ila waking’ang’ania muwaache waende na tutawafuata huko huko,”