Home Michezo TANZANIA POLISI YAMNASA KIPA WA SIMBA SC

TANZANIA POLISI YAMNASA KIPA WA SIMBA SC

0

MANYIKA Peter Manyika ambaye ni mlinda mlango amekamilisha dili lake la kujiunga na Polisi Tanzania kwenye usajili wa dirisha dogo unaotarajiwa kufungwa kesho, Januari 15, saa sita usiku.

Manyika amesaini kandarasi ya mwaka mmoja kuitumikia timu hiyo ya Polisi Tanzania iliyo chini ya Malale Hamsini.

Kabla ya kujiunga na Polisi Tanzania, Manyika alikuwa anakipiga ndani ya klabu ya KCB ya Kenya pia aliwahi kuichezea timu ya Simba na Singida United alipokuwa Bongo.