Home Mchanganyiko MAAFISA WAANDAMIZI WA JESHI KUTOKA CHUO CHA ULINZI CHA TAIFA, NDC WAFANYA...

MAAFISA WAANDAMIZI WA JESHI KUTOKA CHUO CHA ULINZI CHA TAIFA, NDC WAFANYA ZIARA YA MAFUNZO BUNGENI JIJINI DODOMA

0

Katibu wa Bunge, Ndg. Stephen Kagaigai (katikati) akiongoza mazungumzo kati ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi kutoka Chuo cha Ulinzi cha Taifa, NDC (kushoto) na Wakurugenzi wa Idara na Vitengo kutoka Ofisi ya Bunge (kulia) walipokutana leo katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Idara ya Shughuli za Bunge, Ndg. Nenelwa Wankanga akizungumza na Maafisa Waandamizi wa Jeshi kutoka Chuo cha Ulinzi cha Taifa, NDC (kushoto) na Wakurugenzi wa Idara na Vitengo kutoka Ofisi ya Bunge (kulia) walipowatembelea leo katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma.

Katibu wa Bunge, Ndg. Stephen Kagaigai (kulia) akipokea zawadi kutoka Mkufunzi Mwandamizi na Kiongozi wa Msafara kutoka Chuo cha Ulinzi cha Taifa, NDC, Mhe. Balozi Peter Kallaghe wakati Maafisa Waandamizi wa Jeshi kutoka Chuo cha Ulinzi cha Taifa, NDC na Wakurugenzi wa Idara na Vitengo kutoka Ofisi ya Bunge (hawapo kwenye picha) walipokutana leo kwa mazungumzo na kupatiwa maelezo kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na Bunge katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Kimataifa, Ndg. Daniel Eliufoo (kulia) akiwapatia maelezo Maafisa Waandamizi wa Jeshi kutoka Chuo cha Ulinzi cha Taifa, NDC walipotembelea Ukumbi wa Bunge leo kwa ajili ya kujifunza jinsi Bunge linavyofanya kazi yake.

Katibu wa Bunge, Ndg. Stephen Kagaigai (wanne kushoto mbele) katika picha ya pamoja na Maafisa Waandamizi wa Jeshi kutoka Chuo cha Ulinzi cha Taifa, NDC na Wakurugenzi wa Idara na Vitengo kutoka Ofisi ya Bunge nje ya Ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma. Watatu kushoto mbele ni Mkufunzi Mwandamizi  na Kiongozi wa Msafara kutoka NDC, Mhe. Balozi Peter Kallaghe

(PICHA NA OFISI YA BUNGE)