Home Mchanganyiko JAFO AWATOLEA UVIVU WANAOKANDAMIZA WATUMISHI WA CHINI KEC

JAFO AWATOLEA UVIVU WANAOKANDAMIZA WATUMISHI WA CHINI KEC

0
NA MWAMVUA MWINYI,PWANI
WAZIRI wa TAMISEMI ,Suleimani Jafo, amemuelekeza kaimu mkurugenzi wa shirika la elimu Kibaha,Robert Shillingi ,kusimamia shirika hilo na kuandaa timu ,ili kuwadhibiti baadhi ya wataalamu na watendaji ambao wanajigeuza miungu watu kwa kukandamiza watumishi wa chini .

Aidha amekemea tabia ya baadhi ya maofisa utumishi wanaoandaa miongozo ya roho mbaya na kukwamisha taarifa za watumishi waliojiendeleza.
Akizungumza wakati wa kusheherekea maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa shirika la elimu Kibaha,Jafo alisema kuadhimisha kwa miaka hiyo ni vyema wakatathmini shirika lilipo toka na lilipo ili kujirekebisha changamoto zilizopo.
 
“Menejimenti mnakazi ya acheni tabia ta umimi, ndio jambo kubwa la kulifanya ,wakati mnaadhimisha miaka 50 inapaswa kujitathmini na kuona wapi mlikosea ili shirika lisonge mbele”.
“Endeleeni kusimamia mambo kwakuwa mlipotokea sipo tulipo ,nawapongeza sana mlipofikia ila endeleeni kusimamia machache yaliyobaki”alisema Jafo .
Hata hivyo Jafo alieleza , halihitajiki kuwa shirika ombaomba na anatamani liendelee kukua kiuchumi.

“Tulipita katika kipindi kigumu hususan ya mikataba ya uwekezaji iliyokuwa hailingani na thamani ya mali”
Alifafanua adui ya wataalamu ni wataalamu wenyewe, kuna wataalamu wengine kazi yao kutoa miongozo ya roho mbaya .
“Kizazi cha shirika la elimu kuweni na upendo ,msikandamizane kwenye majukumu yenu ,kwakuwa tunapata taarifa za malalamiko kutoka kwa watumishi wa chini na wengine wanadai wanateswa.”
Kuhusu changamoto ya miundombinu alieleza,serikali tayari imeshatoa Trilioni moja kwa ajili ya elimu bila malipo, na pia kutokana na hali ya shule ya sekondari ya Kibaha kuwa mbaya ilitolewa sh. bilioni moja fedha iliwekezwa kwa kuboresha miundombinu hiyo.
Akitolea ufafanuzi,kero ya usafiri usio wa uhakika ambapo kuna kero ya magari ya abiria hayapiti Tumbi na kusababisha wagonjwa kupata shida ya kutoa gharama za pikipiki au tax alimuelekeza mkuu wa mkoa wa Pwani, kushughulikia suala hilo.
Nae kaimu mkurugenzi wa shirika hilo, Robert Shillingi alitaja ,changamoto ufinyu wa bajeti na uchakavu wa miundombinu .
Mkuu wa mkoa wa Pwani,mhandisi Evarist Ndikilo alisema kuna malalamiko kuhusu changamoto za kiutendaji katika hospital ya Tumbi wa baadhi ya watumishi na kuomba wajirekebishe na badala yake watoe huduma bora.
Ndikilo alieleza kutokana na tatizo la bajeti ni vyema wakatumia ardhi iliyopo chini yao kuiendeleza ili kujiongezea kipato ,hivyo alimuomba Jafo kutilia msukumo kupata kibali serikalini,TAMISEMI cha andiko lililoandikwa ili waendeleze ardhi iliyopo kiuchumi.