Home Mchanganyiko RAIS WA ZANZIBAR DK. SHEIN AFUNGUA DARAJA LA KIBONDEMZUNGU BARABARA YA FUONI...

RAIS WA ZANZIBAR DK. SHEIN AFUNGUA DARAJA LA KIBONDEMZUNGU BARABARA YA FUONI ZANZIBAR.

0

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Msimamizi wa Mradi Ujenzi la Kibondemzungu.Eng.Cosmas Masolwa, akitowa maelezo ya kitaalum ya ujenzi huo, wakiwa katika daraja hilo baada ya ufunguzi wake uliofanyika leo,9-1-2020, ikiwa ni shamrashamra za Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar.(Picha na Ikulu)  

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akikagua daraja hilo baada ya kulifungua, (kushoto kwa Rais) Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Mhe.Dkt. Sira Ubwa na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.Mhe. Zuberi Ali Maulid na (kulia kwa Rais) Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Ndg.Mustafa Aboud Jumbe, ikiwa ni shamrashamra za kusherehekea Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akikata utepe kuashiria Uzinduzi wa Daraja la Kibondemzungu Wilaya ya Magharibi “B” Unguja, ikiwa ni shamrashamra za Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar , (kulia  kwa Rais) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi , Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dr. Abdalla Juma Mabodi na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar Mhe. Dkt. Sira Ubwa, hafla hiyo imefanyika katika daraja hilo kibondemzungu.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Balozi Seif Ali Iddi, alipowasili katika viwanja vya hafla ya Ufunguzi wa Daraja la Kibondemzungu, ikiwa ni shamrashamra za Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar wakati wa hafla hiyo iliofanyika katika eneo la daraja hilo.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein, akiondoa kipazia kuashiria ufunguzi wa Daraja la Kibondemzungu Fuoni Wilaya ya Magharibi “B” Unguja (kulia kwa Rais) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.Mhe. Balozi Seif Ali Iddi na Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Ndg. Mustafa Aboud Jumbe na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar Mhe Dkt. Sira Ubwa,ikiwa ni shamrashamra za kusherehekea Miaka 56 ya Mapoinduzi ya Zanzibar.(Picha na Ikulu)