Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Masele akizungumza katika mkutano wake na waandishi wa habari Mjini Shinyanga leo Januari 7,2020 wakati akihitimisha rasmi ziara yake kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali na kusikiliza kero za wananchi na kuelezea mafanikio yaliyopatikana jimboni kwa kipindi cha miaka mitano ya ubunge 2015-2020.
Na Kadama Malunde –
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Masele (CCM) ameelezea mafanikio na maendeleo mbalimbali aliyoyafanya jimboni humo kwa muda wa miaka mitano katika nyanja ya elimu, afya, miundombinu, kilimo na mifugo.
Mhe. Masele ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika ameyaeleza hayo leo Jumanne Januari 7,2020 katika mkutano wake na waandishi wa habari mjini Shinyanga katika majumuisho ya ziara yake ya siku 19 jimboni kwake.
Alisema katika ziara yake hiyo kutembelea kata zote 17 za Jimbo la Shinyanga aliyoianza Desemba 21,2019 ameridhishwa na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM katika kuwaletea maendeleo wananchi.
Alisema kwa kutumia fedha za mfuko wa jimbo la Shinyanga Mjini, wahisani na wafadhili pamoja na nguvu ya wananchi wameweza kujenga zahanati katika vijiji mbalimbali,vituo vya afya, maabara kwenye shule za sekondari, matundu ya vyoo, kuunganisha umeme katika kila kata.
Masele alisema pia amefanikisha kujengwa kwa miundombinu ya madaraja, barabara ambapo jumla ya barabara zenye urefu wa kilometa 13 zimejengwa kwa kiwango cha lami na kufungwa taa zinazowaka usiku na katika awamu ya pili jumla ya kilometa 18 za barabara za lami zitajengwa.
“Kiongozi yeyote anapigania masuala ya afya,elimu,miundo mbinu ya umeme,maji,barabara na madaraja. Nimekuwa mstari wa mbele kuyapigania haya katika jimbo langu ndiyo maana leo mnaona mabadiliko ya kimaendeleo yaliyojitokeza.Shinyanga ya leo siyo Shinyanga ya miaka mitano iliyopita.
“Huwezi kutenganisha maendeleo ya Jimbo la Shinyanga na Mbunge wa Jimbo. Nimekuwa nikishirikiana na wananchi,wadau pamoja na viongozi mbalimbali kuhakikisha Shinyanga unakuwa Mji wa Kisasa kwani tunayo mipango thabiti kufanikisha malengo tuliyojiwekea”,alisema Masele.
Mbunge huyo alisema kiu kubwa ya Wana Shinyanga ni kutaka Shinyanga uwe mji wa Kisasa huku akibainisha kuwa zoezi la kusambaza maji,umeme na kujenga barabara za lami linaendelea ili kufikisha huduma kwenye baadhi ya maeneo ambayo hayajafikiwa.
Masele alitumia fursa hiyo kuwaondoa hofu wananchi ambao wamekuwa wakidai kuwa haonekani Jimboni akisema hali hiyo inatokana na majukumu aliyopewa katika Bunge la Afrika huku akibainisha kuwa licha ya majukumu hayo amekuwa akitekeleza vyema majukumu yake kama Mbunge kutumikia wananchi wake.
“Ninatekeleza vyema majukumu yangu kama Mbunge na nimekuwa nikifanya kazi zangu kwa ushirikiano mkubwa na viongozi mbalimbali wakiwemo madiwani na viongozi wa serikali ili kuhakikisha ahadi zangu kwa wananchi zinatekelezeka”,alisema Masele.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Masele akizungumza katika mkutano wake na waandishi wa habari Mjini Shinyanga leo Januari 7,2020 wakati akihitimisha rasmi ziara yake kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali na kusikiliza kero za wananchi jimboni kwake.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Masele akizungumza katika mkutano wake na waandishi wa habari Mjini Shinyanga leo Januari 7,2020.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Masele akizungumza katika mkutano wake na waandishi wa habari Mjini Shinyanga leo Januari 7,2020.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Masele akizungumza katika mkutano wake na waandishi wa habari Mjini Shinyanga leo Januari 7,2020.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Masele akizungumza katika mkutano wake na waandishi wa habari Mjini Shinyanga leo Januari 7,2020.
Waandishi wa habari wakiandika dondoo muhimu wakati Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Masele akizungumza katika mkutano wake na waandishi wa habari Mjini Shinyanga leo Januari 7,2020
Waandishi wa habari wakimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Masele akizungumza katika mkutano wake na waandishi wa habari Mjini Shinyanga leo Januari 7,2020.
Waandishi wa habari wakimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Masele akizungumza katika mkutano wake na waandishi wa habari Mjini Shinyanga leo Januari 7,2020.
Picha zote na Kadama Malunde