Home Mchanganyiko BARAZA LA VIJANA LAKUTANA KATIKA KIKAO CHA ROBO YA PILI ZANZIBAR

BARAZA LA VIJANA LAKUTANA KATIKA KIKAO CHA ROBO YA PILI ZANZIBAR

0

Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Vijana Zanzibar Wakiskiliza ajenda za kikao cha Baraza la Watendaji la Vijana robo ya pili, wa pili (Kulia) ni Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Taifa Khamis Rashid Kheri  Kikao kilichofanyika  Ofisi ya Vijana huko Mwanakwerekwe Wilaya ya Magharib “B”.

Mjumbe wa Baraza la Vijana Zanzibar Kheri Hassan akichangia Baadhi ya Ajenda zilizowasilishwa katika Kikao cha Baraza la Watendaji la Vijana robo ya pili huko Ofisi ya Vijana Mwanakwerekwe Wilaya ya Magharib “B”.

Mjumbe wa Baraza la Vijana kutoka Pemba Mwinyi hamadi Othman akielezea juu ya kuhamasisha Vijana wa Pemba kujiunga na Mabaraza ya Vijana huko Ofisi za Baraza hilo Mwanakwerekwe Mjini Zanzibar.

……………….

Na Kijakazi Abdalla,Maelezo        

Kuanzishwa kwa Mabaraza ya Vijana Zanzibar kumewawezesha vijana kupiga hatua mbalimbali ambayo inayomuezesha kijana kuweza kutoa maamuzi yaliyo sahihi.

Hayo ameyasema Mkurugenzi Maendeleo ya Vijana Zanzibar Mwanaidi Mohd Ali katika kikao cha robo ya pili kilichofanyika kwenye ukumbi wa Mkutano wa Baraza la Utamaduni Mwanakwerekwe.

Amesema kuanzishwa kwa mabaraza ya vijana kumewezesha vijana kuimarisha kwa kutoa maamuzi ambayo yameweza kufikia malengo ya kuwapatia maendeleo katika Nyanja tofauti.

Aidha amesema kuwa azma ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ni kuona vijana wanaweza kujikomboa katika maisha hasa ikiwemo suala la kiuchumi,kijamii na kisiasa.

Vilevile Mkurugenzi huyo amesema kuwa mabaraza ya vijana yamekuwa na fursa mbalimbali zikiwemo kupata mafunzo ya ufundi na miradi ya kimaendeleo ambayo imekuwa ikizisaidia vijana katika kujikwamua kimaisha.

Nae Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Zanzibar Khamis Rashid Kheri amesema Serikali kupitia mabaraza ya vijana kumewezesha kusimamia vijana 150 kwa kila Wilaya kuweza kuwapatia mafunzo ya ufundi ili kuweza kukabiliana na maisha ya kila siku.

Aidha amesema katika kuona vijana wameweza kuwa na maamuzi sahihi ambayo yamewezesha vijana kuingia katika fursa za kugombania uongozi ili kutekeleza demokrasia.

Nae Mjumbe wa Baraza la Watendaji Taifa Pemba Mwinyi Hamad Othman amesema mabaraza ya vijana yamekuwa na mchango mkubwa kwa vijana kwa taifa kwani vijana wengi wameweza kujiajiri  kupitia miradi ya mabaraza.