Home Michezo SIMBA SC HAIKAMATIKI LIGI KUU BARA YAICHAPA 2-0 NDANDA FC,YAISUBIRI YANGA

SIMBA SC HAIKAMATIKI LIGI KUU BARA YAICHAPA 2-0 NDANDA FC,YAISUBIRI YANGA

0

Vinara wa Ligi Kuu Tanzania bara Wekundu wa Msimbazi Simba wameendelea kuuwasha moto baada ya leo kuichapa 2-0 Ndanda Fc kutoka Mtwara mchezo uliomalizika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

 Francis Kahata aliwanyanyua mashabiki wa Simba  dakika ya 13 akifunga bao kwa mpira wa adhabu nje kidogo ya 18 baada ya Sharaf Shiboub kuchezewa rafu.

Akitokea Benchi winga hatari Deo Kanda alifunga bao la pili mnamo dakika ya 83  akiwa ndani ya 18 baada ya beki wa Ndanda kugonga shuti lililopigwa na Gadiel Michael .

Kwa matokeo hayo Simba imefikisha pointi 34 ikiwa imecheza mechi 13 huku Yanga wakiwa nafasi ya pili kwa pointi 24 wakicheza mechi 11,Januari 4,2020 Tanzania itasimama kwa dakika 90 pale watani wa jadi watakapokutana uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Ligi hiyo itaendelea kesho katika uwanja wa Sheikh Abeid jijini Arusha Singida United ambao wapo kwenye nafasi ya mwisho watakuwa wenyeji wa Azam Fc.