Home Michezo MASHINDANO YA AKINA MAMA KUMEKUCHA 2019 YAWA KUVUTIO MJINI MUSOMA

MASHINDANO YA AKINA MAMA KUMEKUCHA 2019 YAWA KUVUTIO MJINI MUSOMA

0
 Mwenyekiti wa UWT Taifa Mama Gaudesia
Kabaka akizungumza wakati akifungua Mashindano ya Wakina mama yaliyopewa jina la Kumekucha akina mama wa Musoma 2019
Mlezi wa Chama cha mchezo
wa Netball Mkoani Musoma mjini Wakili Suzana Senso ambaye pia ni Mdhamini wa Mashindano hayo akizungumza wakati wa ufunguzi
Mwenyekiti wa UWT Taifa Mama Gaudesia
Kabaka kulia akifuatilia mashindano hayo kushoto ni Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Mara Wegesa Hassan
Mlezi
wa Chama cha mchezo
wa Netball Mkoani Musoma mjini Wakili Suzana Senso ambaye pia ni
Mdhamini akifuatilia mashindano hayo ambaye pia ni miongoni mwa
waandaaji wa mashindano hayo akifuatilia kwa umakini
Wadhamini
wakiwa na washindi wa kwanza kutoka kushoto watatu ni Naibu Meya wa  Musoma mjini Mr. Igwe  na wanne kutoka kulia ni
Mkurugenzi wa Uhuru Hospitali  Derick Nyasebwa
moja kati ya mechi zikiendelea uwanjani
Mlezi
wa Chama cha mchezo
wa Netball Mkoani Musoma mjini Wakili Suzana Senso ambaye pia ni
Mdhamini katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya timu
zinazoshiriki mashindano hayo
Mwenyekiti wa UWT Taifa Mama Gaudesia
Kabaka katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wadau wa michezo mjini Musoma wa pili kulia ni
Mlezi
wa Chama cha mchezo
wa Netball Mkoani Musoma mjini Wakili Suzana Senso ambaye pia ni
Mdhamini mashindano hayo kushoto ni Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Mara
Wegesa Hassan

Kamati ya maandalizi ikiongozwa na Mwenyekiti wa netball Musoma mjini Bi Godviler

NA MWANDISHI WETU, MUSOMA

 

MASHINDANO
ya Wakina mama yaliyopewa jina la Kumekucha akina mama wa Musoma 2019
yamekuwa kivutia kukibwa Musoma Mjini huku waaandaji wakihaidi kuendelea
kuyafanya kila mwaka lengo kutoa fursa kwa wanawake kuonyesha vipaji vyao kupitia huko.

 

Mgeni rasmi kwenye mashindano hayo alikuwa Mama Gaudesia
Kabaka Mwenyekiti wa UWT Taifa ambapo alipongeza waandaaji wa mashindano
hayo na kusema  hii ni mara ya kwanza kwa mashindano hayo kutokea Mara
Kwani haijawahi kutokea na yameendeshwa kwa kufuata kanuni za mashindano
kwa michezo.

 

Michezo
ambayo ilifanyika kwenye mashindano hayo ni Netball, wakina mama
kukimbiza kuku, kuvuta kamba na kukimbiza magunia ikiwa ni mkakati wa
kuhakikisha tunaendelea vipaji vya wakina mama.

 

Mashindano hayo yaliandaliwa na Mlezi wa Chama cha mchezo
wa Netball Mkoani Musoma mjini Wakili Suzana Senso alisema kwamba
wameamua kuandaa mashindano hayo kwa sababu wakina  mama wanakuwa wamesahaulika kwenye michezo hasa Netball.

 

Akizungumza
wakati wa mashindano hayo Mlezi wa Chama cha Mchezo wa Netball mkoani
Musoma Wakili Suzana alisema kwamba alisema wameamua kuanzisha
mashindano hayo ili kutoa fursa kwa wakina mama nao kuweza kuonyesha
vipaji vyao walivyonavyo.

 

“Kikubwa
zaidi niwaambie kwamba tumeamua kufanya mashindano hayo kwa wakina mama
waweze kuonyesha vipaji vyao kwani mabonanza mengi hayausishi wakina
mama hilo ndilo ambalo limewasukuma kuwasiliana na
Naibu Meya wa Musoma Mjini Bwana Igwe na tukaona tuandae hicho kitu
tunamshukuru Mungu kimekwenda vizuri”Alisema

 

Hata
hivyo alisema kwamba pia wana mpango wa kuandaa mashindano mengine ya
wakina mama yatakayofanyika Machi 8 mwakani lengo kubwa ni kuhakikisha
wanawawezesha kushiriki kwenye mashindano mbalimbali nao waweze
kuendeleza vipaji vyao.

 

Hata
hivyo aliyashukuru makampuni mbalimbali yaliyojitokeza kuunga mkono
mashindano hayo kwa kuyasaidia ambao ni Uhuru Hospitali, Chama cha
Netbally Mkoa Musoma na Meya wa Manispaa Musoma, UWT Mkoa.

 

Naye
kwa upande wake Mkurugenzi wa Uhuru Hospitali Dkt Derick Nyasebwa
alisema kwamba wameamua kushiriki mashindano hayo ya wakina mama na
wamefurahi kwa sababu yeye pia ni mzaliwa lakini kwa niaba ya Uhuru
Hospitali .

 

Alisema
waliamua kuhakikisha wanashiriki kwenye michezo  hiyo kwani kufanya
hivyo ni kampeni kubwa zinazoendelea nchini kutoka wizara ya
Afya,maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto inayoongozwa na  Waziri
wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu
kuhakikisha wanaelimisha watu kuepukana na magonjwa yasiyoambuliza
kupitia michezo ni njia nzuri ya kuepukana na kusukari,saratani na
msukumo wa damu kuwa juu.