Waziri wa ardhi Nyumba na maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akitoa maagizo ya kumvua cheo Grarson Godfrey Mkurugenzi wa Miliki Shirika la Nyumba (NHC) baada ya kugundua uzembe kazini kuhusu upangishaji wa nyumba ya NHC iliyopo Muhimbili jijini Dar es salaam.
…………………………………………
Waziri wa ardhi Nyumba na maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amemvua cheo Grarson Godfrey Mkurugenzi wa Miliki Shirika la Nyumba (NHC) baada ya kugundua uzembe kazini na kusababisha upotevu wa fedha za serikali kutokana na moja ya nyumba iliyopo Muhimbili jijini Dar es salaam kupangishwa kinyume cha uKAKA HUJAMBO POLE KWA USUMBUFU NAKUOMBA UTUMIE HIZI CODES KWENYE ILE STORY YA NHC ZA AWALI ZINA MAKOSA KIDOGO MKUU taratibu wa shirika hilo.
Akizungumza katika eneo la tukio Waziri Lukuvi leo amemwagiza Mkurugenzi wa Shirika hilo Dk.Maulid Banyani kumuondoa katika nafasi hiyo na kuangalia wote waliohusika au kushiriki kwa upotevu wa fedha hizo kuchukuliwe hatua za kinidhamu.
Mtu mmoja ambaye hakutajwa jina lake amewapangisha wafanyabiashara mbalimbali katika jengo hilo wakimlipa kiasi cha shilingi laki moja 100,000 kila mmoja kwa mwezi huku yeye akililipa shirika la nyumba (NHC) kiasi cha shilingi elfu ishirini na Nne 24,000 kwa mwezi.
Wapangaji hao wamepanga katika jengo hilo kwa muda wa miaka 13 na wamekuwa wakimlipa mtu huyo kiasi hicho kila mwezi jambo ambalo linalikosesha mapato shirika la nyumba pia Mamlaka ya Mapato TRA haikusanyi kodi ya serikali kutokana na udanganyifu huo uliofanyika kwa muda mrefu na kusababisha upotevu wa fedha nyingi za serikali.
Waziri Lukuvu ameongeza kuwa kama Mkurugenzi huyu wa Miliki katika shirika la nyumba (NHC) ameshindwa kuchukua hatua kwa ubadhirifu uliopo kwenye nyumba ya hapa Muhimbili tu. ataweza kugunda na kuchukua hatua katika majengo yaliyopo nchi nzima maana yake ni fedha nyingi zinapotea kwa uzembe huu.
“Huyu ameshindwa kwenda na kasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. DK. John Pombe Magufuli ambaye anataka kila fedha ya serikali ikusanywe na kuleta maendeleo kwa watanzania wanyonge” Amesema Lukuvi.
Wakati huohuo Waziri wa ardhi Nyumba na maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amemuagiza Mkurugenzi wa Shirika la nyumba NHC Dk. Maulid Banyani kumpa taarifa ya kiufundi na kitaalamu itakayokuwa imejitosheleza kuhusu sababu za kuchelewa kumalizika kwa ujenzi wa Machinjio ya Vingunguti ambayo Rais. Dk. John Pombe Magufuli aliagiza ujenzi ukamilike Disemba 31 2019 wakati alipotembelea mradi huo.
Ameongeza kwamba sababu hizo zielezwe wazi na ziwe ni za msingi ili baada ya hapo yeye amtaarifu Mh. Rais Dk. John Pombe Magufuli kuhusu ucheleweshwaji huo kabla mwezi januari mwaka ujao.
“Lazima nijiridhishe nione sababu zenyewe kama ni za msingi, Kitaalam na Kiufundi ili nami nimtaarifu Ras kuhusu kuchelewa kukamilika kwa mradi huu” Amesema Lukuvi.
Hata Hivyo Waziri Lukuvi amelipongeza shirika hilo kwa utekelezaji wa mradi huo wa machinjio ya Vingunguti kwa kasi na viwango vizuri ambao ni wa 35 kati ya miradi yote ambayo Shirika la hilo linatekeleza nchi nzima ambapo amesema mradi huo unaendelea vizuri.
Waziri wa ardhi Nyumba na maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akiangalia leseni za wajasiriamali hao ambao wamepangishwa katika nyumba ya NHC kinyume cha utaratibu kulia ni Mkurugenzi wa Shirika hilo Dk.Maulid Banyoni na katikati ni Said Seif Mketo mmoja wa wapangaji.
Waziri wa ardhi Nyumba na maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akimsikiliza Mkurugenzi wa Shirika la nyumba NHC Dk.Maulid Banyani na katikati ni Said Seif Mketo mmoja wa wapangaji.
Waziri wa ardhi Nyumba na maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akimsikiliza mmoja wa wapamgaji katika nyumba hiyo Said Seif Mketo alipokuwa akimuelezea jinsi ambavyo wamekuwa wakinyanyaswa na mtu aliyewapangisha kulia ni Mkurugenzi wa Shirika la nyumba NHC Dk.Maulid Banyani.
Waziri wa ardhi Nyumba na maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akizungumza na Mkurugenzi wa Shirika la nyumba NHC Dk.Maulid Banyani wakati alipokuwa akikagua ujenzi wa jengo la machinjio ya nyama Vingunguti ambalo linajengwa na NHC.
Waziri wa ardhi Nyumba na maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akzungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukagua ujenzi huo kulia ni Mkurugenzi wa Shirika la nyumba NHC Dk.Maulid Banyani
Waziri wa ardhi Nyumba na maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akitoa maagizo kwa Mkurugenzi wa Shirika la nyumba NHC Dk.Maulid Banyani wakati alipotembelea na kukagua ujenzi wa machinjio hayo Vingunguti.
Waziri wa ardhi Nyumba na maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akizungumza na Meneja Mawasiliano wa Shirika la Nyumba la Taifa Muungano Saguya kushoto ni Mkurugenzi wa Shirika la nyumba NHC Dk.Maulid Banyani