Spika wa Bunge la Tanzania, Mhe. Job Ndugai (katikati) akizungumza na Naibu Spika wa Bunge la Watu wa China, Mhe. Ji Bingxuan (kulia) alipomtembelea Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Balozi wa China nchini, Mhe. WANG Ke.
Spika wa Bunge la Tanzania, Mhe. Job Ndugai pamoja na ujumbe wake (kulia) katika mazungumzo na Naibu Spika wa Bunge la Watu wa China, Mhe. Ji Bingxuan pamoja na ujumbe wake (kushoto) Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.
Spika wa Bunge la Tanzania, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akimkabidhi zawadi ya picha ya Jengo la Bunge, Naibu Spika wa Bunge la Watu wa China, Mhe. Ji Bingxuan (kulia) mara baada ya mazungumzo Jijini Dar es Salaam.
Spika wa Bunge la Tanzania, Mhe. Job Ndugai (watatu kushoto) na Naibu Spika wa Bunge la Watu wa China, Mhe. Ji Bingxuan (wa tatu kulia) wakizindua Mpango wa ushirikiano wa Asasi za kiraia za Tanzania na za China Jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki (wa kwanza kulia), Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya UKIMWI, Mhe. Oscar Mukasa (wa kwanza kushoto) na Balozi wa China nchini Mhe. WANG Ke (wa pili kushoto).
Spika wa Bunge la Tanzania, Mhe. Job Ndugai akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mpango wa ushirikiano wa Asasi za Kiraia za Tanzania na za China Jijini Dar es Salaam.
Spika wa Bunge la Tanzania, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akizungumza na Naibu Spika wa Bunge la Watu wa China, Mhe. Ji Bingxuan (kulia) kabla ya uzinduzi wa Mpango wa ushirikiano wa Asasi za Kiraia za Tanzania na za China Jijini Dar es Salaam.
Spika wa Bunge la Tanzania, Mhe. Job Ndugai (kushoto) katika picha ya pamoja na Naibu Spika wa Bunge la Watu wa China, Mhe. Ji Bingxuan (kulia) mara baada ya uzinduzi wa Mpango wa ushirikiano wa Asasi za Kiraia za Tanzania na za China Jijini Dar es Salaam.
Spika wa Bunge la Tanzania, Mhe. Job Ndugai (kulia) akiagana na Naibu Spika wa Bunge la Watu wa China, Mhe. Ji Bingxuan (katikati) mara baada ya uzinduzi wa Mpango wa ushirikiano wa Asasi za Kirai za Tanzania na za China Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Balozi wa China nchini, Mhe. WANG Ke.