Home Mchanganyiko SACP MUSLIM AMEWATAKA MADEREVA KUWA WAANGALIFU BARABARANI

SACP MUSLIM AMEWATAKA MADEREVA KUWA WAANGALIFU BARABARANI

0

*******************************

 Madereva wametakiwa kuwa waangalifu katika kuhakikisha usalama wa abiria hasa katika kipindi hiki cha mwisho wa mwaka kutokana na uzoefu wa huko nyuma kwamba kipindi kama hiki hutokea ajali nyingi.

 

Ameyasema hayo Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Nchini, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Fortunatus Muslim akizungumza na madereva wa mabasi yanayokwenda mikoani.

 

Muslim aliwataka madereva kuzingatia suala la afya na kuwasisitiza kutosimamisha magari sehemu zisizo rasmi kwaajili ya abiria kujisaidia, amesema suala hilo maarufu kama kuchimba dawa ni kosa kisheria na sio salama kwa wananchi kujisaidia vichakani na wanaweza pia kuwasababishia ajali kutokana na madereva kusimamisha magari maeneo ambayo sio salama, badala yake amewataka kusimamisha magari maeneo ambayo yamejengwa vyoo na yameandaliwa rasmi kwa abiria kupata huduma hiyo.