Home Mchanganyiko RAIS MHE.DKT.MAGUFULI AFUNGUA JENGO LA MAHAKAMA YA WILAYA YA CHATO PAMOJA NA...

RAIS MHE.DKT.MAGUFULI AFUNGUA JENGO LA MAHAKAMA YA WILAYA YA CHATO PAMOJA NA KUZINDUA UJENZI WA KITUO CHA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI CHA WILAYA YA CHATO MKOANI GEITA

0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe pamoja na Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma, Spika wa Bunge Job Ndugai pamoja na Waziri wa Katiba na Sheria Balozi Agustine Mahiga kuashiria ufunguzi wa Jengo la Mahakama ya Wilaya ya Chato mkoani Geita.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma mara baada ya kufungua jengo la Mahakama ya Wilaya ya Chato lililopo Mlimani Chato mkoani Geita.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua eneo la Mapokezi katika jengo jipya la Mahakama ya Wilaya ya Chato lililopo eneo la Mlimani Chato mkoani Geita mara  baada ya kulifungua.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mke wake Mama Janeth Magufuli wapili kutoka kulia waliokaa, Spika wa Bunge Job Ndugai watano kutoka kulia waliokaa, Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma wanne kutoka kushoto waliokaa pamoja na viongozi wengine wa Mkoa pamoja na viongozi wa Kidini mara baada ya kufungua jengo jipya la Mahakama ya Wilaya ya Chato.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi wa Chato mara ya kufungua jengo la Mahakama la Wilaya ya Chato.

Moja ya Vyumba vya Mahakama hiyo ya Wilaya ya
Chato kama inavyoonekana pichani.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe kuashiria uwekaji wa Jiwe la Msingi mradi wa ujenzi wa Kituo cha Jeshi la Zimamoto la Wilaya ya Chato mkoani Geita.

Sehemu ya Jengo la Kituo cha Jeshi la Zimamoto na
Uokoaji cha Wilaya ya Chato kilichowekewa Jiwe la Msingi leo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli. PICHA NA IKULU