Home Mchanganyiko BODI YA WAKURUGENZI WA TANESCO IMERIDHISHWA UTEKELEZAJI WA MRADI WA KUFUA UMEME...

BODI YA WAKURUGENZI WA TANESCO IMERIDHISHWA UTEKELEZAJI WA MRADI WA KUFUA UMEME WA MAJI WA JULIUS NYERERE (MW 2115)

0

Mwenyekiti Wa Bodi Ya Wakurugenzi Wa Shirika La Umeme Tanzania (TANESCO) Dkt Alexander Kyaruzi (aliyeinama) akimuelekeza jambo furani Mhandisi Steven Manda,ambaye pia ni mratibu wa Mradi wa Kufua Umeme wa maji wa Julius Nyerere (MW 2115) walipotembelea mradi huo.

Bodi ya wakurugenzi wa shirika la umeme Tanzania Tanesco wakiwa katika Mradi wa Kufua Umeme wa Maji wa Julius Nyerere (MW 2115) December 17.

Mratibu Wa Mradi wa kufua umeme wa maji wa Julius nyerere(MW 2115)  Mhandisi Steven Manda akitoa maelezo kwa Mwenyekiti Wa Bodi Ya Wakurugenzi Wa Shirika La Umeme Tanzania (TANESCO) Dkt Alexander Kyaruzi wakati alipotembelia mradi huo December 17.

*******************************

Na Farida Saidy ,Morogoro

Mwenyekiti Wa Bodi Ya Wakurugenzi Wa Shirika La Umeme Tanzania (TANESCO) Dkt Alexander Kyaruzi Amesema Hatomvumilia Mtu Yeyote Atakayebainika Kuhujumu Mradi Wa Kufua Umeme Wa Julius Nyerere (MW 2115) Uliopo Katika Mikoa Ya Morogoro Na Pwani.

Dkt Kyaruzi Aliyasema Hayo December Disemba 17 alipotembelea Shughuli Mbalimbali Zinazoendelea Kutekelezwa Katika Mradi Huo, Ambapo Aliambatana Na Wajumbe Wa Bodi Hiyo, Alisema Ametembelea Na Kujionea Shughuri Mbalimbali Zinazoendelea Katika Mradi Huo Na kusema Ameridhishwa Na Hatua Uliofikiwa.

“Anayejijua anataka kuhujumu huu mradi bora akimbie nchi” alisema Dkt Kyaruzi.

Katika Hatua Nyingine Dkt Kyaruzi Aliwataka Wafanyakazi Kufanya Kazi Kwa Ushirikiano Ili Kuendana Na Kasi Iliyopo, ambapo Alisema Kwa Sasa Bodi Imeridhishwa Na Kasi Inayoendelea Katika Mradi Huo Pamoja Na Kuwataka Wafanyakazi Wote Kufanyakazi Kwa Ushirikiano Ili Uweze Kukamilika Kwa Muda Uliokusudiwa. 

Hata hivyo Walitembelea Maeneo Mbalimbali Ikiwemo Makazi Ya Watumishi, Ujenzi Wa Barabara ,Na Njia Ya Kuchepushia Maji Kwaajili Ya Ujenzi Rasmi Wa Bwawa Hilo, na kuthibitisha kuridhishwa Na Kazi Inayoedelea Katika Ujenzi Wa Mradi Huo.

Kwa upande Wake Mkurugenzi Mtendaji Wa Shirika La Umeme Tanzania, Dkt Tito Mwinuka Alisema Kuwa Kasi Wanaoendelea Nao Wakandarasi Inalidhisha Na Wanatarajia Kumaliza Mradi Huo Kabla Ya wakati.

Nae Mratibu Wa Mradi Huo Mhandisi Steven Manda Alisema Kuwa Hadi Sasa Mradi Huo Umefikia Asilimia Kumi (10%)Ya Utekelezwaji Wake,Huku Ujenzi Wa Madaraja kwa sasa Ukiwa Umefikia Asilimia 90, Na jingine Likiwa Limemalizika Kwa
Asilimia Mia Moja.

Hata Hivyo Baadhi Ya Wajumbe Wa Bodi Hiyo Ya Wakurugenzi Wa TANESCO walioambatana na Mwenyekiti Huyo Akiwemo Makamu Mwenyekiti Wa Bodi Balozi James Nzagi Na Dkt Gemma Modu Wamesema Kuwa Wapo Tayari Kushirikiana Kwa Pamoja Ili Mradi Huo Ukamilike Kwa Haraka Kama Ilivyukusudiwa.