Home Mchanganyiko BODI TISA ZA MAZAO KUUNGANISHWA ILI KUUNDA BODI TATU PEKEE-WAZIRI HASUNGA

BODI TISA ZA MAZAO KUUNGANISHWA ILI KUUNDA BODI TATU PEKEE-WAZIRI HASUNGA

0

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza na viongozi wa vyama vya ushirika katika ukumbi wa Wilaya ya Tandahimba akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Mtwara, jana tarehe 13 Disemba 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Sehemu ya wakulima wa korosha wakifatilia hotuba ya Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza na viongozi wa vyama vya ushirika katika ukumbi wa Wilaya ya Tandahimba akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Mtwara, jana tarehe 13 Disemba 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza na viongozi wa vyama vya ushirika katika ukumbi wa Wilaya ya Tandahimba akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Mtwara, jana tarehe 13 Disemba 2019.
Na Mathias Canal, Wizara ya
Kilimo-Mtwara
Serikali
imedhamiria kuziunganisha Bodi sita za mazao zilizopo chini ya Wizara ya Kilimo
na kuwa na Bodi tatu ili kuongeza ufanisi wa kiutendaji
Waziri wa
Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo jana tarehe 13 Disemba 2019 wakati akizungumza na
viongozi wa vyama vya ushirika katika ukumbi wa Wilaya ya Tandahimba akiwa
katika ziara ya kikazi Mkoani Mtwara.
Waziri
Hasunga amesema kuwa kumekuwa na Bodi nyingi lakini matokeo ya kiutendaji hayaakisi
wingi huo hivyo ili kuboresha majukumu yake na kuwa na weledi katika kazi Bodi
hizo zitaunganishwa.
Amesema
kuwa Bodi saba zitaunganishwa na kuunda Mamlaka moja ya kusimamia mazao ya
kimkakati ambayo ni pamoja na Kahawa, Pamba, Mkonge, Tumbaku, Pareto, Korosho,
Alizeti na zao la mchikichi.
Waziri
Hasunga amesema kuwa mabadiliko hayo yatakayozihusisha Bodi hizo yatapelekea
kuundwa kwa idara za kusimamia kila zao.
Bodi
nyingine ya pili itasimamia mazao ya nafaka, mboga mboga na matunda (Cereal and
Horticulture Authority) pamoja na Bodi ya Sukari itakayosalia kujitegemea.
Amesema, kuwa
na Bodi nyingi kumepelekea usimamizi kuwa mgumu kadhalika kuwa na Bodi chache
kutaimarisha ufanisi na uwezo wa kuwasimamia watendaji wake.
Sambamba
na hayo Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) amesema kuwa Wizara ya Kilimo
ipo katika mchakato wa kupitia upya sheria ya Ushirika pamoja na Shirika la
ukaguzi wa vyama vya Ushirika-COASCO ili kuimarisha sheria na kuwa na usimamizi
madhubuti wa mali za wananchi kwenye Ushirika.
Waziri
Hasunga yupo mkoani Mtwara kwa ajili ya ziara ya kikazi ambapo awali
alitembelea mkoa wa Pwani na Lindi
kwa ajili ya kukagua hali ya
uuzaji wa korosho msimu wa 2019/2020, kukagua hatua zilizofikiwa za malipo ya
wakulima wa korosho zilizonunuliwa na serikali msimu wa mwaka 2018/2019 na
kukagua skimu za umwagiliaji.