Home Mchanganyiko Kampeni ya Tunaboresha Sekta ya Afya Yatinga Hospitali ya Mirembe Mkoani Dodoma

Kampeni ya Tunaboresha Sekta ya Afya Yatinga Hospitali ya Mirembe Mkoani Dodoma

0
Mkurgenzi wa Hospitali ya Mirembe na Taasisi ya Isanga, Dkt. Erasmus Mndeme akizungumza kuhusu mafanikio ya Taasisi anayoingoza ndani ya kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Tano, chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli alipotembelewa na Maafisa Habari na Mawasiliano wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Afya) na Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo leo jijini Dodoma. Ziara hiyo ni muendelezo wa Kampeni ya Tunaboresha Sekta ya Afya inayoratibiwa na Wizara ya Afya kwa kushirikiana na taasisi zilizo chini yake kuelezea maboresho yanayofanywa katika sekta hiyo.
Mkuu wa Taasisi ya Afya na Sayansi Shirikishi Dodoma (DIHAS), Bi. Rehema Mligo akifafanua jambo mbele ya Maafisa Habari na Mawasiliano wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto(Idara Kuu ya Afya) na Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo walipotembelea Taasisi hiyo leo jijini Dodoma. Ziara hiyo ni muendelezo wa Kampeni ya Tunaboresha Sekta ya Afya inayoratibiwa na Wizara ya Afya kwa kushirikiana na taasisi zilizo chini yake kuelezea maboresho yanayofanywa katika sekta ya Afya chini ya utawala wa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli. Taasisi hiyo inatoa masomo ya katika fani ya Uuguzi katika ngazi ya Stashahada.

Mkuu wa Taasisi ya Afya na Sayansi Shirikishi Dodoma (DIHAS), Bi. Rehema Mligo akielezea namna ambavyo wanafunzi wa uuguzi wanaosoma katika Taasisi hiyo wanavyopatiwa mafunzo ya katika maabara ya kisasa ya ujuzi iliyopokatika taasisi hiyo mbele ya Maafisa Habari na Mawasiliano wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto(Idara Kuu ya Afya) na Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo walipotembelea Taasisi hiyo leo jijini Dodoma.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto(Idara Kuu ya Afya), Bw. Gerald Chami(kushoto) akisikiliza kwa makini maelezo kuhusu huduma ya Maktaba inayotolewa na Taasisi hiyo toka kwa Mkuu wa Taasisi ya Afya na Sayansi Shirikishi Dodoma (DIHAS), Bi. Rehema Mligo (katikati) wakati wa ziara ya Maafisa Habari na Mawasiliano wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto(Idara Kuu ya Afya) na Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo leo jijini Dodoma. Kulia ni Mkutubi wa Maktaba hiyo, Andrew Gerald. Ziara hiyo ni muendelezo wa Kampeni ya Tunaboresha Sekta ya Afya inayoratibiwa na Wizara ya Afya kwa kushirikiana na taasisi zilizo chini yake kuelezea maboresho yanayofanywa katika sekta ya Afya chini ya utawala wa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
Muonekano wa Jengo jipya la Bweni la wanafunzi wa Taasisi ya Afya na Sayansi Shirikishi Dodoma (DIHAS) ambalo linauwezo wa kuchukua wanafunzi 270. Jengo hilo limekuwa msaada mkubwa kwa wanafunzi wa taasisi hiyo ambapo limetatua changamoto ya wanafunzi kukaa nje ya chuo. Ambapo awali bweni lililokuwepo lilikuwa na uwezo wa kulaza wanafunzi 180 tu kati ya wanafunzi 400 wanaosoma chuo hicho. Taasisi hiyo inatoa masomo ya katika fani ya Uuguzi katika ngazi ya Stashahada.
Kiti maalumu cha kutolea huduma ya tiba ya magonjwa ya kinywa na meno ambayo inatolewa katika Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe.
Moja ya majengo yaliyokarabatiwa katika Hospitali ya Mirembe ambayo kihistoria ilianzishwa na Mjerumani o miaka ya 1920.
Jengo la kihistoria kuhusu Hospitali ya Mirembe mkoani Dodoma ambalo lilijengwa mwaka 1926. Jengo hili lilijengwa na wakoloni wa Kijerumani kwa sasa linatumiwa na wagonjwa wa afya ya akili walikatika uangalizi wa karibu.
Baadhi ya mafundi wakishona sare za wanafunzi wa fani ya Uuguzi wanaosoma katika Taasisi ya Afya na Sayansi Shirikishi Dodoma (DIHAS) wakiendelea na kazi ya ushonaji was are hizo ikiwa ni maandalizi ya sare kwa ajili ya wanafunzi kuendea kwenye mafunzo kwa vitendo.
Baadhi ya wanafunzi wa Taasisi ya Afya na Sayansi Shirikishi Dodoma (DIHAS) Stashahada ya Uuguzi mwaka wa pili wakiwa darasani leo jijini Dodoma.(Picha na Wizara ya Afya)