Home Mchanganyiko WAFANYAKAZI WA SBL WAJUMUIKA PAMOJA KUSHEREKEA KUAGA MWAKA 2019

WAFANYAKAZI WA SBL WAJUMUIKA PAMOJA KUSHEREKEA KUAGA MWAKA 2019

0
Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Bia ya Serengeti wa kiwanda cha Mwanza, wakifurahia kujumuika pamoja katika sherehe za kuaga mwaka 2019 na kuukaribisha mwaka 2020 zilizofanywa na kampuni hiyo jijini Mwanza,
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni ya Bia ya Serengeti, John Wanyancha,akizungumza kwenye hafla ya kuwapongeza wafanyakazi wa kampuni hiyo jijini Mwanza kwa utendaji wao.

……………….

Mwanza

Wafanyakazi wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) katika viwanda vya Moshi, Dar es Salaam na Mwanza, jana walijumuika pamoja kusherehekea msimu wa sikukuu kwa kuaga mwaka 2019 na kuukaribisa mwaka 2020.

“SBL imeajiri takribani wafanyakazi 800 kupitia ajira za moja kwa moja kwenye viwanda vyake huku ikitengeneza ajira zisizo za moja kwa moja kwa maelfu ya Watanzania, alisema mkurugenzi wa Mahusiano kwa Ummawa kampuni hiyo John Wanyancha kwenye maadhimisho ya sherehe hizo katika kiwanda cha Mwanza.

“Katika maadhimisho ya leo, wafanyakazi wetu wanaburudika kwa kupata chakula na vinywaji pamoja na burudani za kwaya kutoka makanisa yaliyo jirani na viwanda vyetu vitatu. Pia wanapata nafasi ya kusikiliza hotuba za kutia moyo na kujenga kutoka kwa menejimenti ya kampuni.

Malengo yetu yanaendelea kubaki kuwa mwajiri bora. Tutaendelea kuboresha maslahi ya wafanyakazi kwa kuwa tunaamini ni jambo la msingi katika kuwapa motisha na hivyo kufanya kazi kwa bidi zaidi,” aliongeza Wanyancha 

SBL ni mzalishaji wa Serengeti Premium Lager, bia inayotengenezwa na kimea kwa asilimia 100 na pia SBL ni msambazaji wa pombe kali zenye viwango vya kimataifa ambazo ni pamoja na Johnnie Walker, Ciroc, Smirnoff vodka, White Horse, J&B na nyinginezo. 

Kwa upande mwingine, Serengeti Premium Lager ni mdhamini wa timu ya taifa, Taifa Stars huku Serengeti Lite ikiwa mdhamini wa ligi ya soka ya wanawake. Ukiachana na michezo, SBL inafadhili miradi mbali mbali inayolenga kusaidia jamii katika maeneo mbali mbali nchini  kwenye maeneo kama upatikanaji wa maji safi na salama, unywaji wa kistarabu pamoja na kutoa ufadhili wa masomo ya elimu ya juu kwa wanafunzi wanaotoka katika familia zenye kipato duni sana.   

Kwa mujibu wa Wanyancha, kampuni ya SBL inawasaidia wakulima wazawa wanaolima mazao yanayotumiwa na viwanda vyake kwenye uzalishaji wa bia kama shayiri, mahindi na uwele. Kupitia mpango wa kusaidia wakulima, wakulima wanapata mbegu bora pasipo malipo, ushauri wa kitaalamu wa bure kutoka kwa maofisa ughani na pia huunganishwa na taasisi za fedha kwa ajili ya kupata mikopo inayposaidia kuongeza uzalishaji wao.

Mwaka 2018, SBL ilinunua tani za ujazo 17,000 za nafaka kutoka kwa wakulima wazawa ambazo ni sawa na asilimia 70 ya jumla ya mahitaji yake kwa mwaka. Nafaka hizi hununuliwa kutoka kwa mtandao wa wakulima 400 walio chini ya mpango wa kampuni hiyo na pia yapo malengo ya kuongeza idadi.