Home Mchanganyiko SERIKALI HAITOPANGA BEI ELEKEZI KWENYE MAZAO–WAZIRI HASUNGA

SERIKALI HAITOPANGA BEI ELEKEZI KWENYE MAZAO–WAZIRI HASUNGA

0

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo tarehe 11 Disemba 2019 wakati akizungumza kwenye kikao kazi kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Lindi wakati akiwa katika ziara ya siku mbili mkoani humo kukagua hatua zilizofikiwa za malipo ya wakulima wa korosho msimu wa mwaka 2018/2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Baadhi ya wakulima wa korosho Mkoani Lindi wakifatilia hotuba ya Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) tarehe 11 Disemba 2019 wakati akizungumza kwenye kikao kazi kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Lindi wakati akiwa katika ziara ya siku mbili mkoani humo kukagua hatua zilizofikiwa za malipo ya wakulima wa korosho msimu wa mwaka 2018/2019.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe Godfrey Zambi akisisitiza jambo tarehe 11 Disemba 2019 wakati akizungumza kwenye kikao kazi kilichoongozwa na Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) wakati akiwa katika ziara ya siku mbili mkoani humo kukagua hatua zilizofikiwa za malipo ya wakulima wa korosho msimu wa mwaka 2018/2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo tarehe 11 Disemba 2019 wakati akizungumza kwenye kikao kazi kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Lindi wakati akiwa katika ziara ya siku mbili mkoani humo kukagua hatua zilizofikiwa za malipo ya wakulima wa korosho msimu wa mwaka 2018/2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akipokelewa na Mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe Godfrey Zambi tarehe 11 Disemba 2019 wakati alipowasili mkoani humo akiwa katika ziara ya siku mbili kukagua hatua zilizofikiwa za malipo ya wakulima wa korosho msimu wa mwaka 2018/2019.
Na Mathias Canal, Wizara ya
Kilimo- Lindi
Serikali
imesema kuwa haitopanga bei elekezi kwenye mazao mbalimbali ya kilimo kuanzia
msimu ujao wa kilimo wa mwaka 2019/2020 badala yake itaacha soko liamue.
Waziri wa
Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo tarehe 11 Disemba 2019 wakati
akizungumza kwenye kikao kazi kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi za Mkuu wa
Mkoa wa Lindi wakati akiwa katika ziara ya siku mbili mkoani humo kukagua hatua
zilizofikiwa za malipo ya wakulima wa korosho msimu wa mwaka 2018/2019.
Waziri
Hasunga amesema kuwa katika kipindi kirefu serikali imekuwa ikijihusisha kupanga
bei elekezi ya mazao jambo ambalo huchochea sintofahamu kwa wakulima wakati bei
ya mazao katika soko la Dunia inaposhuka.
Amesema
kuwa serikali itahakikisha kuwa inasimamia kwa weledi sekta ya kilimo ili
kuhakikisha kuwa kunakuwa na uhalali katika biashara ya mazao ya wakulima kwa
kuangalia mwenendo wa soko la Dunia, uwezo wa wanunuzi na kiasi kitakacholipwa
kwa wakulima.
“Tumepanga
bei huko kwenye Pamba tumekoswakoswa, Tukapanga kwenye kahawa mambo mabaya,
kwenye tumbaku mambo mabaya, tumesema wakulima wenyewe wanapolima ndio wapange
bei” Alisema Mhe Hasunga
Katika
upande mwingine Waziri Hasunga amesema kuwa serikasli kupitia wizara ya Kilimo
inajipanga kuhakikisha kuwa inawasimamia maafisa ugani kwa weledi mkubwa ili
waweze kuwasaidia wakulima ili kuwa na uzalishaji wenye tija.
Amesema
kuwa wizara imekusudia kuweka utaratibu utakaowawezesha maafisa ugani hao kuwa
na fomu maalumu zitakazopima utendaji kazi wao.
Mhe
Hasunga amesema kuwa ofisi za maafisa ugani ni mashambani hivyo  ni lazima wapimwe ufanisi wao wa kazi kwa
kwenda mashambani na jinsi walivyowasaidia wakulima.
Kwa
upande mwingine waziri Hasunga amezitaja taasisi za fedha kutofanya vizuri
katika kuwasaidia wakulima ili kupata mikopo yenye riba nafuu jambo
litakalowanufaisha na kuongeza uwezekano wa kuwa na zana bora za kilimo
kadhalika pembejeo bora.
Katika
ziara hiyo Waziri Hasunga amebaini baadhi ya wakulima waliouza korosho zao kwa
serikali katika msimu wa kilimo wa mwaka 2018/2019 kutolipwa fedha zao jambo
ambalo limemshangaza Kwakuwa serikali ilishatoa fedha zote kwa ajili ya
kuwalipa wakulima hao.