Home Michezo PSG,REAL MADRID ZATINGA 16 BORA KWA USHINDI MNONO LIGI YA MABINGWA ULAYA

PSG,REAL MADRID ZATINGA 16 BORA KWA USHINDI MNONO LIGI YA MABINGWA ULAYA

0

Mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil, Neymar akishangilia baada ya kuifungia  Paris St Germain bao la tatu dakika ya 46 katika ushindi wa 5-0 dhidi ya Galatasaray kwenye mchezo wa Kundi A Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa jana Uwanja wa Parc des Princes mjini Paris. Mabao mengine ya PSG yalifungwa na Mauro Icardi dakika ya 32, Pablo Sarabia dakika ya 35, Kylian Mbappe dakika ya 63 na Edinson Cavani kwa penalti dakika ya 84. PSG imeongoza kundi kwa pointi zake 16, ikifuatiwa na Real Madrid iliyomaliza na pointi 11 baada ya kuifunga Club Brugge 3-1 na jana na zote zinakwenda 16 Bora

Vinicius Junior akishangilia baada ya kuifungia Real Madrid bao la pili dakika ya 64 katika ushindi wa 3-1 dhidi ya wenyeji, Club Brugge kwenye mchezo wa Kundi A Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa jana Uwanja wa Jan Breydel mjini Brugge. Mabao mengine ya Real Madrid yalifungwa na Rodrygo dakika ya 53 na Luka Modric dakika ya 90 na ushei, wakati la Club Brugge lilifungwa na Hans Vanaken dakika ya 55. Real imamaliza nafasi ya pili nyuma ya PSG na zote zinakwenda hatua ya 16 Bora