Home Mchanganyiko WATU WANNE WAKAMATWA KWA TUHUMA ZA KUWATEKA WATOTO WAWILI CHALINZE-WANKYO

WATU WANNE WAKAMATWA KWA TUHUMA ZA KUWATEKA WATOTO WAWILI CHALINZE-WANKYO

0

NA MWAMVUA MWINYI,PWANI

WATU wanne wanaotuhumiwa kuwateka nyara watoto wawili na kudai fedha kiasi cha sh. milioni mbili wamekamatwa na polisi baada ya kutuma ujumbe wa vitisho kwenye simu ya mama wa watoto hao ambao ni wafamilia moja.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kamanda wa polisi mkoani humo Wankyo Nyigesa alisema kuwa watu hao walikamatwa baada ya kutumiwa kiasi cha fedha.

Nyigesa alisema kuwa tukio hilo lilitokea Desemba 4 mwaka huu majira ya saa 2:00 asubuhi huko Bwilingu wilaya ya kipolisi Chalinze watoto wawili mmoja wa kike mwenye umri wa miaka (8) na mwingine wa kiume (5) ambao ni wanafunzi wa shule ya msingi Bwilingu.

“Tulipata taarifa kupotea kwa watoto hao tarehe 5 Desemba na tulianza kufuatilia kwa mitandao ya simu iliyoonekana kutuma ujumbe kwa mama wa watoto hao Claudia Fute simu hiyo yenye namba 0715 648672 iliyosajiliwa kwa jina la Subira Kasenga,” alisema Nyigesa.

Alisema kuwa simu hii ilituma jumbe nyingi za vitisho kwa mama mzazi na kutaka atumiwe fedha haraka kiasi hicho vinginevyo angewadhuru watoto hao na kuwafanya lolote hata kuondoa uhai wao.

“Kwa kutumia namba hiyo pia tulibaini namba nyingine ya Farida Gabriel iliyokuwa ikisisitiza mtekaji aendelee kushikilia watoto kea sababu pesa itatumwa tu na kumsisitizia Kasenga kuwa akomae kwani mama wa watoto anatafuta fedha atume,” alisema Nyigesa.

Aidha alisema kuwa katika kuhakikisha wanafanikisha katika kufanikisha kukamatwa wahusika walituma kiasi cha shilingi 400,000 kwa mtuhumiwa na ndipo wakati akitoa alikamatwa na polisi.

“Watuhumiwa waliokamatwa ni Husna Hussein Mwinyigoha (18) ambaye ndiye aliyeteka watoto akitumia jina la Subira pia namba yake nyingine ni 0693838511 na 0719648672 iliyosajiliwa kwa jina la Subira Kasenga,Farida Gabriel (34) mwenye namba ya simu 0716461161 na 0784641456, Said Thomas mwenye namba 0692986611 na Miraji Mrisho Mbega,” alisema Nyigesa.

Alibainisha watuhumiwa watafikishwa mahakamani mara upelelezi utakapokamilika ili wajibu tuhuma zinazowakabili za utekaji watoto hao wadogo.