Home Mchanganyiko WANA JUKWAA LA CHALINZE WATOA MSAADA WA MIFUKO YA SARUJI 120

WANA JUKWAA LA CHALINZE WATOA MSAADA WA MIFUKO YA SARUJI 120

0
NA MWAMVUA MWINYI,CHALINZE
WANA-Jukwaa la Chalinze 
Tunayoitaka linaloundwa na wapenda maendeleo wa Chalinze Bagamoyo Pwani,wamemkabidhi mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete risiti ya  sh. milioni 1.8 kwa ajili ya mifuko 120 ya saruji kwa ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa na ofisi ya walimu,katika shule ya msingi Kibiki.
Akimkabidhi risiti hiyo ,mwenyekiti wa Jukwaa Alhaj Hamisi Nassoro, alisema mchango huo ni wa wana-Jukwaa hilo.
Alisema, Jukwaa linaundwa na wadau wa maendeleo, na kwamba wamedhamilia kupambana na changamoto za kielimu.
Aidha Nassoro aliomba fedha za maendeleo na wananchi zitumike kwa maslahi ya jamii.
“Hapa ni mwanzo wa shughuli zetu za kuipeleka mbele Chalinze yetu, lakini  katika hili wana-Jukwaa tunaomba tupatiwe taarifa za kina, za uwepo wa tetesi za matumizi mabaya ya zaidi ya shilingi milioni miamoja, zinazotajwa kutumika pasipokufuatwa kwa utaratibu,” alisema Alhaj Nassoro.
Ridhiwani aliwashukuru wana-Jukwaa na kuwaomba wanajukwaa kulitumia kwa kuchochea maendeleo na sio kuwa sehemu ya kuleta migongano kwa wana-Chalinze.
“Katika Jukwaa kuna baadhi ya mijadala mingine haileti tija, utaona mtu unatuma jambo ambalo wazi linalenga kuchafuana kisiasa, hili jambo sio zuri mimi niko tayari hata kukaa na sturi hapa mbele nikawapa ruksa ha kuuliza maswali yenu yote, kisha nikayajibu,” alisema Ridhiwani.
 Kwa upande wake diwani Lufunga alisema kuwa katika kuunga mkono uboreshaji elimu katani humo, halmashauri ya Chalinze na Mbunge huyo wameshaipatia fedha za kujenga vyumba vya madarasa katika shule zilizomo katani humo, pia amewashukuru wana-Jukwaa kwa moyo huo.
Nae mmoja wa wajumbe Omary Mtiga alisema kuwa wao katika Kata ya Kibindu walikuwa na Jukwaa kama hilo walilolipatia jina la Kibindu Tunayoitaka, ambalo limeleta mafanikio makubwa katika uboreshaji wa shule katani humo.
Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Magreth Kileo anawashukuru wadau hao kwa kuguswa na mahitaji ya shule hiyo, na kwamba msaada huo utapunguza adha ya upungufu wa vyumba