Home Teknolojia DATS MFUMO WA KIJERUMANI AMBAO UNAMRAHISISHIA MWANAGENZI KUELEWA KWA VITENDO

DATS MFUMO WA KIJERUMANI AMBAO UNAMRAHISISHIA MWANAGENZI KUELEWA KWA VITENDO

0

************************************

NA EMMANUEL MBATILO

Dual Apprenticeship Training system.(DATS) ni mfumo ambao mwanafunzi(mwanagenzi) kuweza kusoma wiki kadhaa chuoni,na kutumia wiki kadhaa kwa mafunzo viwandani on job Training.

Mfumo hutumia mfumo wa “Block release” ambapo Mwanagenzi, hutakiwa kuja chuoni kwa muda wa wiki saba(7) chuoni,baada ya hapo hurudi kiwandani (On job Training )kwa muda wa wiki kumi na mbili (12) .ambapo kwa mwaka zipo block tatu amazo humfanya Mwanagenzi huyu kusoma kwa Jumla ya wiki 52.

Mafunzo haya hutolewa kwa muda wa miaka Mitatu(3),ili kumfanya mwanagenzi kuwa mahiri.

Mfumo huu umekuwa chachu ya maendeleo hasa katika viwanda na kuendana na kauli mbiu ya Serikali ya awamu ya Tano ya Uchumi wa Viwanda kwa Maendeleo ya nchi.

Akizungumza na Fullshangwe blog katika Kongamano baina ya Serikali na Wafanyabiashara na Wawekezaji Nchini lililofanyika katika viwanja vya Maonesho vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam, Mratibu Msaidizi wa Mafunzo hayo ya DATS ( VETA) Bw. Challange Fihili amesema kuwa mfumo DATS umekuwa ukifanyika nchini Ujerumani kwa muda mrefu sana ili kuwajengea umahiri wafanyakazi kwenye viwanda mbalimbali, mfumo huu kwao ulileta maendeleo makubwa sana katika nchi hiyo.Ndipo Serikali ya Tanzania ikaamua kuuleta pia hapa nchini mwaka 2011 kuweza kuleta chachu ya maendeleo ya Viwanda nchini.

Bw.Challange amesema kuwa mfumo huo umsaidia kuondoa mapungufu kati ya mahitaji ya soko (viwanda) na mtoa mafunzo ( Reduce mismatch betwee Training and labour market needs), hivyo mfumo huo umeweza kutatua changamoto hiyo kwani makampuni yanayonufaika na mfumo huo mfumo huu yamefikia 155 mpaka sasa.

“Mfumo huo ulianza kwa majaribio kwa awamu ya kwanza kwa muda wa mwaka 2011 mpaka 2013, wakati kwa awamu ya pili ilianza mwaka 2013 mpaka 2016 lakini baadae mwaka 2017 wakapanua wigo na waongeze muda ili angalau ikifika 2018 kutuachia tuendelee”. Amesema Bw.Challange

Aidha, Bw.Challange amesema kuwa Mwaka 2018, walianza kutekeleza mfumo huo, wao kama VETA , mfumo wa mafunzo na mpaka sasa wanaendelea vizuri na wanategemea mwaka 2020 hadi 2025 kuingiza viwanda 2000 kwenye mfumo huu wa mafunzo.

Ameongeza kuwa kwa sasa wapo wanagenzi ( Apprentices)224 ambao Tayari wameajiriwa na viwanda hivyo.Na secta za mafunzo zilizotekelezwa na pamoja na Umeme (Electrical installation) na ufundi magari(Automotive) kwa chuo cha Changombe Dsm, uhotelia (Hospitality) VETA moshi,na Agromechanics pale Manyara- Babati.

Vilevile amesema kuwa wanatarajia kufungua mafuzo kwenye Secta za Hotelia Pale VETA Mtwara na Plumbing (mabomba) pale Chuo cha VETA Mbeya kwa mwaka 2020.

Bw.Challenge ametoa wito kwa wenye viwanda kuomba kushirikiana kuhakikisha mfumo huu unaimarika kwa maendeleo ya nchi na kuongeza nafasi za ajira kwa vijana wetu kwa maendeleo endelevu.

Kwa upande wake mwanagenzi VETA, Bw.Shafii Kamgisha, amesema mafanikio ambayo ameyapata kupitia mfumo huu wa Darts, ni kwamba anajifunza vitu vingi kwa vitendo kwahiyo anakuwa anafahamu mifumo mingi ya gari kuanzia injini ya gari na mambo mengine yanayohusiano na gari.

“Huu mfumo huu ni mzuri unamuwezesha mwanafunzi kuelewa na pia kumuahakikishia mwanafunzi uhakika wa kupata sehemu ya kujifunzia (field practice)”.Amesema Bw.Kamgisha.

“Uhakika wa kuajiliwa upo maana wengi waliomaliza mafunzo haya kwa mfumo huu wameajiliwa tena katika makampuni mazuri, yeye tu anachagua ni sehemu gani anaweza kwenda”.Ameongeza Bw.Kamgisha