Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizindua matrekta matatu yaliyonunuliwa na Wakala wa Mbegu (ASA) kwa ajili ya kuongeza ufanisi wa uzalishaji mbegu bora wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja Mkoani Morogoro, jana tarehe 4 Disemba 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akikabidhi mbegu Bora zilizozalishwa na Wakala wa Mbegu (ASA) kwa ajili ya kuongeza ufanisi wa mazao Visiwani Zanzibar wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja Mkoani Morogoro, jana tarehe 4 Disemba 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akikagua mbegu bora zilizozalishwa na Wakala wa Mbegu (ASA) wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja Mkoani Morogoro, jana tarehe 4 Disemba 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akikagua mbegu zinazozalishwa na Wakala wa Mbegu (ASA) wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja Mkoani Morogoro, jana tarehe 4 Disemba 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akikata utepe kuashiria uzinduazi wa matrekta matatu yaliyonunuliwa na Wakala wa Mbegu (ASA) kwa ajili ya kuongeza ufanisi wa uzalishaji mbegu bora wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja Mkoani Morogoro, jana tarehe 4 Disemba 2019.
Na
Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Morogoro

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga
(Mb) ametangaza kuifuta Bodi ya Wakala wa Mbegu (ASA) endapo itashindwa
kusimamia majukumu yake ipasavyo ikiwa ni pamoja na kuzalisha mbegu za kilimo
zipatazo Tani 5000 katika msimu wa kilimo wa mwaka 2019/2020.

Ametoa kauli hiyo jana tarehe
4 Disemba 2019 wakati akizungumza na watumishi wa Taasisi hiyo mara baada ya
kutembelea Mkoani Morogoro akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja ambapo
amesema kuwa tishio hilo litahusisha pia Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mbegu.

Amesema kuwa pamoja na ASA
kuongeza eneo la uzalishaji wa mbegu kutoka hekta 9890 mpaka kufikia hekta
10,115.2 lakini bado uzalishaji ni mdogo kwani ASA inazalisha Tani 1440 pekee
huku zaidi ya asilimia 85 ya watanzania wanaojihusiaha na kilimo wakiwa na
uhitaji wa mbegu.

Waziri Hasunga amesema kuwa matrekta
matatu mapya yaliyonunuliwa na ASA pamoja na zana zake kama vile Boom Spayer,
majembe matatu mapya na Planter tatu mpya yanapaswa kutumika ipasavyo kwa ajili
ya kuongeza uzalishaji wa mbegu bora.

“Sisi kama nchi tunahitaji Tani
100,086 za mbegu na mpaka sasa hivi uwezo wetu wa kuzalisha ndani na kuagiza
nje hauzidi Tani 57,000 sasa mahitaji ni makubwa watu wanataka mbegu bora
lakini uzalishaji bado upo chini” Amesisitiza Mhe Hasunga

Waziri Hasunga amesema kuwa mbegu
bora ndio msingi na muhimili wa kilimo hivyo ili kubadilisha kilimo kutoka kujikimu
na kuwa kilimo chenye tija na cha kibiashara ni lazima kuwa na uzalishaji
mkubwa wa ndani ya nchi.

Aliongeza kuwa serikali
itaiwezasha ASA kuongeza vituo vya usambazaji wa mbegu kutoka vitano ambavyo
vinatumika sasa mpaka kuwa vituo 10 ili kuwarahisishia wakulima kupata mbegu
katika maeneo yao.

Kadhalika, waziri Hasunga
amemtaka Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mbegu (ASA) kuhakikisha kuwa anatatua
changamoto alizozibainisha kwenye taarifa yake ikiwemo ukosefu wa mtaji wa
kutosha, kutokuwa na hifadhi ya mbegu ya Taifa, ukosefu wa miundombinu ya
umwagiliaji, upungufu wa vitendea kazi na uhaba wa vituo vya kusambaza mbegu.

Changamoto zingine ni
upungufu wa magari ya kusambaza mbegu, uchakavu wa mitambo ya kuchakata mbegu, na
upungufu na uchakavu wa maghala ya kuhifadhia mbegu.

Wakala wa Mbegu (ASA)
ulianzishwa chini ya sheria ya wakala za serikali sura ya 245 na kufanyiwa
marekebisho mwaka 2009 na kuzinduliwa rasmi tarehe 23 Juni, 2006 ikiwa ni
Taasisi inayounganisha sekta ya umma na binafsi katika mfumo wa uzalishaji na
usambazaji wa mbegu bora.