Home Michezo Msuva kubaki Difaa El Jadida hadi 2021

Msuva kubaki Difaa El Jadida hadi 2021

0

********************************

NA EMMANUEL MBATILO

Kiungo Mshambuliaji wa klabu ya Difaa El Jadida na timu ya taifa ya Tanzania, Simon Msuva amesaini mkataba mpya wa miaka miwili ndani ya klabu yake. Mkataba utakaomuweka kwenye klabu hiyo hadi mwaka 2021.

Msuva alikuwa anahusishwa kurudi katika klabu yake ya zamani ya Yanga lakini kwa upande wake ametamani kubaki katika klabu hiyo ambayo inashiriki ligi kuu ya nchini Morroco.