Home Mchanganyiko TANESCO KUINGIA KWENYE BIASHARA YA UMEME YA KIMATAIFA

TANESCO KUINGIA KWENYE BIASHARA YA UMEME YA KIMATAIFA

0

Mratibu wa mradi Mhandisi Peter kigadya,akitoa maelezo kwa bodi ya Tanesco ambayo ilifanya ziara ya kukagua  ujenzi wa kituo cha kupozea umeme cha Zuzu kilichopo jijini Dodoma. 

Sehemu ya ujenzi wa kituo cha kupozea umeme cha Zuzu kilichopo jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la umeme nchini Tanesco Mhandisi.Alexander Kyaruzi,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukagua ujenzi wa kituo cha kupozea umeme cha Zuzu kilichopo jijini Dodoma.

…………….

Na.Alex Sonna,Dodoma

SHIRIKA la umeme nchini (TANESCO) limesema kuwa  maboresho yanayofanywa kwenye Gridi ya taifa ya kuunganisha mtandao wa umeme nchi jirani za kenya,Burundi na Zambia kutaliwezesha kuwa kiungo muhimu cha biashara ya kimataifa ya kuuza na kununua umeme kati ya nchi za kaskazini na kusini mwa bara la Afrika.

Hayo yalibainishwa na Mwenyekiti wa bodi ya Shirika la umeme nchini Tanesco Mhandisi.Alexander Kyaruzi wakati akikagua ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme cha Zuzu kilichopo Dodoma katika mradi wa wa njia ya umeme ya Msongo Kilovolt 4000.

Kyaruzi amesema kuwa  kituo hicho kinatarajia kukamilika mapema mwakani kimeongezewa uwezo wa uzalishaji toka megawati 48 hadi 748,maboresho hayo pia yamefanywa kwenye vituo vilivyoko katika mradi ili kukidhi mahitaji ya umeme ndani na nje ya nchi.

Amesema kuwa biashara hiyo itakuwa imara kwa sababu kutakuwa na vyanzo vingi vya umeme kutoka kwenye gesi,na kwingineko ambapo wanaamini vitasaidia kwa kiasi kikubwa katika ujenzi wa viwanda.

‘kutakuwa na viwanda vingi ambavyo vitajengwa ndio maana tumeviongezea uwezo wa kuzalisha umeme ili uweze kujitosheleza katika viwanda vilivyopo,”amesema Kyaruzi.

Aidha amesema kuwa  umeme ni muhimu kukamilika katika muda uliopangwa kutokana na kwamba taifa hivi sasa linaekea katika uchumi wa kati wa viwanda hivyo ni lazima viwanda viwe na umeme.

Kwa upande wa mratibu wa mradi huo mhandisi Peter kigadya amesema kuwa lengo la kujiunga na nchi jirani katika Gridi hiyo ni kutokana na kutaka kuendeleza biashara ya umeme toka hapa nchini na nchi jirani.

Mhandisi Kigadya amesema moja ya faida ambazo zitapatikana kupitia muunganiko huo ni pamoja na Tanzania ikikosa umeme itanunua kwa jirani lakini majirani wakikosa Tanzania itawauzia umeme kutoka hapa nchini.

Aidha amesema kuwa  wataendelea na mfumo wa upanuzi wa vituo hivyo lengo ikiwa ni kutaka kuvipa uwezo wa kufanya kazi kwa kiasi kikubwa na kuongeza huo utaenda katika mikoa mbalimbali hapa nchini.

Akitolea ufafanuzi juu ya ujenzi wa vituo hivyo katika awamu hii alisema wanatarajia kutumia sh milion 120 katika mikoa minne ya Dodoma,Singida,Iringa na Shinyanga.

Amesema kuwa ujenzi wa kituo cha kupozea umeme cha Zuzu kinatarajia kukamilika mwishoni mwa Januari mwakani.