Home Siasa PEMBA YAAMUA, CCM NDIO CHAGUO LAO KWA SASA.

PEMBA YAAMUA, CCM NDIO CHAGUO LAO KWA SASA.

0

*********************************

Mchana wa leo tarehe 03 Desemba, 2019 Katibu Mkuu wa CCM akiendelea na ziara yake Kisiwani Pemba Mkoa wa Kusini amepokea wanachama wapya 950 kutoka vyama Mbalimbali vya siasa.

Ambapo kwa mujibu wa utaratibu wa CCM wanachama hawa wapya wamefuzu mafunzo ya itikadi na Imani ya CCM, hivyo leo wamekabidhiwa kadi ya Uanachama na kuwa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

“Nimekuja kufunga mitambo ya ushindi wa CCM Pemba, na nimefanya hivyo Unguja na nilishafanya hivyo Bara, na kupokea wanachama hawa ni moja ya mitambo ambayo ikianza kulipuka kuna watu watasema wanaibiwa kura”. Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Bashiru Ally.

“Mitambo hii nitafunga mingi zaidi Pemba, ambapo nitapokea wanachama wengi zaidi na sasa mnaona, leo tumepokea wanachama 950 na bado wanakuja wengi zaidi”. Amesisitiza

Kabla ya kupokea wanachama hao, Katibu Mkuu ameshiriki ujenzi wa ofisi ya CCM Tawi la Kendwa, ambapo amewaunga mkono wanachama wa Tawi hilo kwa kuchangia mifuko ya sementi 100.