Home Mchanganyiko KAMISHNA WA MAADILI AWATAKA VIONGOZI WA UMMA MKOA WA GEITA KUZINGATIA MATAKWA...

KAMISHNA WA MAADILI AWATAKA VIONGOZI WA UMMA MKOA WA GEITA KUZINGATIA MATAKWA YA SHERIA YA MAADILI

0

Kamishna wa Maadili Jaji (Mst) Harold Nsekela akifafanua jambo pale alopotembelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita katika ziara aliyoifanya iliyokuwa na lengo la kuwakumbusha Viongozi wa Umma wa Mkoa wa Geita kuzingatia matakwa ya Sheria ya Maadili.  Kushoto kwa Kmaishna na Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Luhumbi akifuatiwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita, Bw. Denis Bandisa. Wakwanza kushoto ni Bw. Waziri Kipacha ambaye ni Katibu Idara ya Ukuzaji Maadili Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

Kamishna wa Maadili Jaji (Mst) Harold Nsekela akiwasilisha mada ya maadili iliyojikita katika Mgongano wa Maslahi, Ujazaji wa Fomu na Ahadi ya Uadilifu kwa Viongozi wa Umma wa Mkoa wa Geita katika ziara aliyoifanya mkoani humo yenye lengo la kuwakumbusha Viongozi wa Umma kuhusu uzingatiaji wa matakwa ya Sheria ya Maadili.