Home Mchanganyiko TAARIFA KWA UMMA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOANI MWANZA

TAARIFA KWA UMMA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOANI MWANZA

0

JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LINAWASHIKILIA WATU WATANO KWA TUHUMA ZA KUHUSIKA KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE KATIKA MAUAJI YA WATU WATATU. WATU WALIOUAWA NI; 1.DOTTO CONSTANTINE, @ MAKAYANGA, MIAKA 19, MSUKUMA,  2.BAKAR I,s/o UMRI KATI YA MIAKA 20 HADI 25 NA MTU WA TATU HAKUFAHAMIKA JINA, UMRI KATI YA MIAKA 20 HADI 25, WOTE WANADAIWA KUWA WAKAZI WA NYAKABUNGO “A”, WALIUAWA KWA KUPIGWA FIMBO NA MAWE KATIKA SEHEMU MBALIMBALI ZA MIILI YAO NA KUNDI LA WATU WANAODAIWA KUJIJICHUKULIA SHERIA MKONONI BAADA YA KUWATUHUMU KUJIHUSISHA NA VITENDO  VYA WIZI NA UBAKAJI.

TUKIO HILO LIMETOKEA TAREHE 01.12.2019 MAJIRA YA 19:45HRS, HUKO MTAA WA NYAKABUNGO “B”, WILAYANI NYAMAGANA, HII NI BAADA YA VIJANA HAO (MAREHEMU) KUPITA MTAA WA NYAKABUNGO ‘B”, NDIPO WALIKUTANA NA WATU WALIOANZA  KUWAKIMBIZA NA BAADAE MWENYEKITI WA MTAA HUO AITWAYE ABDULKADIRI YUNUSU @ JACOBO, MIAKA 55, MHAYA, ALIPIGA FIRIMBI HUKU AKITAMKA KUWA WATU HAO NI WEZI NA BAADAE WATU WALIWAKAMATA NA KUWAFUNGA KAMBA KISHA KUWAPIGA MAWE NA FIMBO HADI WAKAPOTEZA MAISHA.

WATUHUMIWA WALIOKAMATWA KUHUSIANA NA MAUAJI HAYO NI 1.ABDULKADIRI YUNUSU @ JAKOBO, MIAKA 55, MHAYA, MWENYEKITI WA MTAA WA NYAKABUNGO “B”, 2.EZEKIEL ZEPHANIA @ SENSO, MIAKA 35, MKURYA, AMBAYE ALIWAFUNGA KAMBA MAREHEMU, 3.ATHUMAN CHACHA, MIAKA 45, MKURYA, 4. RAMADHAN ATHUMAN, MIAKA 48, NA 5. HAMIS PETER, MIAKA 22, MKURYA, WOTE WALIHUSIKA KUWAFUNGA KAMBA MAREHEMU.

JESHI LA POLISI LINAENDELEA NA UPELELEZI WA TUKIO HILONA   UCHUNGUZI UKIKAMILIKA WATAFIKISHWA MAHAKAMANI. AIDHA UFUATILIAJI WA KUWATAFUTA WATU WENGINE WALIOHUSIKA KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE NA TUKIO HILO BADO UNAENDELEA. MIILI YA MAREHEMU IMEHIFADHIWA HOSPITALI YA MKOA SEKOU TOURE KWA AJILI YA UCHUNGUZI NA UTAMBUZI.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA ANATOA ONYO KWA MARA NYINGINE WANANCHI WENYE TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI  WAACHE TABIA HIYO NA WAVIACHIE VYOMBO VYA DOLA VIFANYE KAZI YAKE KAMA MFUMO WA UTAWALA WA SHERIA UNAVYOTAKA .KUFANYA KINYUME KAMA WATUHUMIWA WALIVYOFANYA  NI KOSA LA JINAI, NA MADHARA YAKE NI KUSHITAKIWA MAHAKAMANI 

IMETOLEWA NA:

Muliro J. MULIRO- ACP

KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA.