Home Michezo IROLE FC YAPOKEA KIPIGO CHA 6-1KUTOKA KWA MAFINGA ACADEM KATIKA ASAS SUPER...

IROLE FC YAPOKEA KIPIGO CHA 6-1KUTOKA KWA MAFINGA ACADEM KATIKA ASAS SUPER LEAGUE 2019/2020

0

Waamuzi wa Asas Super League 2019/2020 ambao wamekuwa wakichezesha michezo mingi ya ligi hiyo yenye msisimko mkoani Iringa na nje ya mkoa wa Iringa (picha kutoka maktaba)
Mwenyekiti wa chama cha mpira mkoa wa Iringa Cyprian Kuyava akiwa wasalimia wachezaji wa timu ya Irole fc waliofungwa sita moja na timu ya Mafinga Academy (picha kutoka maktaba)
 
NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
 
Timu ya Irole fc y wilayani
kilolo mkoani Iringa imekuwa timu ya kwanza kupata kipigo kikubwa kuliko timu
zote zinazoshiriki ligi ya Asas Super League 2019/2020 baada ya kupokea kipigo
cha goli sita kwa bila.
 
Timu ya Irole fc inayoshikili
nane bora ya Asas Super League imejikutaka ikikung’utwa goli sita moja na timu
ya Mafinga Academy katika mchezo uliochezwa katika uwanja wa Wambi uliopo
katika uwanjwa wa wilaya ya Mufindi.
 
Ikumbukwe kuwa Irole fc ndio
moja ya timu bora kabisa kushiriki ligi hiyo huku wakionyesha upinzani mkubwa
kwenye hatua za awali za ligi hiyo ambao moja ya mechi ambazo walicheza kwa
kutoa vipigo vingi huku kipigo kikubwa kikiwa kwenye mchezo wao dhidi ya Ismani
fc ambao waliwabugiza tano mchezo ulichezwa kwenye nuwanja wa Irole fc.
 
Tangu timu ya Irole fc itinge
hatua ya nane bora tayari imeshacheza michezo mitatu huku ikitoa sare michezo
miwili huku mmoja akipokea kipigo kikali kutoka kwa Mafinga Academ
 
Katika michezo ambayo imechezwa
siku hii ya leo timu ya Ismani Fc imeendeleza ubabe wake kwa kuitungua goli
moja timu ya kimali fc kutoka katika uwanja wa kijiji cha ruang’a kilichopo
tarafa ya Ismani mkoani Iringa.
 
Na michezomingine itaendelea
siku ya kesho kati ya Nzihi fc ambao watakuwa wanawakaribisha timu ya Mkimbizi
fc kutoka manispaa ya Iringa na mchezo huo utachezwa katika uwanja wa kijiji
cha Nzihi.