Home Michezo NAIBU WAZIRI KUFUNGA MASHINDANO YA GOFU YA TANZANIA ARUSHA

NAIBU WAZIRI KUFUNGA MASHINDANO YA GOFU YA TANZANIA ARUSHA

0

Naibu Waziri wa mambo ya Nje Damas Ndumbaro (KATIKATI) akiwa katika Picha ya pamoja na Viongozi wa Chama cha Gofu tanznaia TGU kabla ya kuingia Uwanjani katikaa mashindano hayo yaliyochukua Siku Tatu .

Baadhi ya Wachezaji kutoka Vilabu Mbalimbali wakiwa tayari kwa ajili ya kuingia katika Mchuano wa mashindo ya Wazi ya Tanzania open katika Uewanja wa Kili jijini Arusha.

……………….

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Mh Damas Ndumbaro anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika ufungaji wa mashindano ya wazi ya Gofu ya Tanzania open yanayofanyika katika Uwanja wa Kili Jijini Arusha.

Akizungumza katika Siku ya Pili ya Mchezo huo  Mwenyekiti wa Chama cha Gofu Tanzania (TGU) Criss Martin alisema Maandalizi yote yamekamilika na kinachosubiriwa ni hitimisho kesho Jumapili  licha ya mvua iliyonyesha Nyakati za mchana.

“ Mvua ilinyesha lakini bahati nzuri haijaathiri kiasi cha kuvunja mchezo licha ya kuchelewesha wachezaji ambao iliwalazimu kujificja kwa ajili ya Mvua na muda kwenda lakini hali ikawa sawa “ Alisema Mwenyekiti wa TGU.

Aidha alisema anawashukuru wadau wote waliofanikisha mashindano haya makubwa wakiwemo Verge Africa ambao wamehakikisha maandalizi yote yamekamilika ikiwemo upatikanaji wa Wadhamini ambao ndi mafanikio ya mashindano.

Kwa upande wake Mchezaji Victor Joseph ameendelea kuipeperusha vyema bendera ya tanznai kwa kuongoza katika wachezaji wa Divisheni A baada ya kupiga 71 nna kuendelea kuongoza na kubakiza matumaini ya Watanzania.

Victor alisema licha ya Mvua lakini bado anaendelea kupambana kuhakikisha kikombe kinabaki Tanznaia kutokana na uwepo wa wachezaji kutoka nchi Nyingine amabao wameshiriki katika Mashindano haya.

Kwa Upande wa Wachezaji wa Kulipwa kutoka Kenya  Dismass Indiza ameendelea kuongoza huku kwa Wachezaji wa Ridhaa Victor joseph wa klabu ya Golf ya  Dar es Salaam Gymkhana wameendelea kufanya vyema.

Kwa upande wake Dismass Indiza alisema mchezo umekuwa mgumu siku ya pili baada ya siku ya kwanza kutokana na mvua na hata ushindani haukuwa wa nguvu kufuatia hali ya hewa lakini matumaini yake yake katika hatua ya mwisho ya fainali  Leo jumapili.