Home Mchanganyiko DKT.BASHIRU ASEMA CCM ITAENDELEA KUENZI MAPINDUZI YA KIJAMII

DKT.BASHIRU ASEMA CCM ITAENDELEA KUENZI MAPINDUZI YA KIJAMII

0

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Dkt.Bashiru Ally Kakurwa, akivishwa skafu na Vijana Maalum wa UVCCM  Wilaya ya Dimani  katika ziara yake katika mkoa wa magharib kichama.

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Dkt.Bashiru Ally Kakurwa,akizungumza na Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Magharib.

BAADHI ya Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Magharib wakimsikiliza mgeni rasmi, Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Dkt.Bashiru Ally Kakurwa huko katika ukumbi wa CCM  Wilaya ya Dimani kichama.

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Dkt.Bashiru Ally Kakurwa, akikagua bidhaa mbali mbali zinazotengenezwa na wajasiriamali wa Mkoa huo huko katika soko la mboga mboga Mombasa Zanzibar.

……………….

NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi  (CCM) Dkt.Bashiru Ally,amesema CCM itaendelea kuenzi Mapinduzi ya kijamaa ili kukuza Uchumi wa nchi.

Hayo ameyasema wakati akizungumza na vyombo mbali mbali vya  Habari mara baada ya kumaliza Kikao cha Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Magharibi.

Alisema chama hicho sio chama cha uchaguzi bali ni Chama cha Mapinduzi ya kijamaa katika kutenda haki kwa kila Mwananchi bila ubaguzi wa dini,rangi na Kabila.

Alisema Mapinduzi ya kisiasa yaliyowakomboa wananchi wa Zanzibar, kutoka katika Karume enzi za uhai waliasisi Mapinduzi ya kijamaa kwa lengo la kuwakomboa wananchi kijamii,kisiasa na kiuchumi.

“Kazi yetu ni kuwatumikia kama tulivyowaahidi wakati wa kuomba ridhaa zao wakati wa kampani za uchaguzi mkuu uliopita na tumetekeleza kwa vitendo maisha ya wananchi yamekuwa mazuri licha ya kuwepo na changamoto ndogo ndogo zinaendea kutatuliwa ili zimalizike kabla ya 2020.”,alisema Dkt.Bashiru. Bashiru.

Akizungumzia mafanikio yaliyopatikana katika ziara yake hiyo katika Mikoa ya Unguja Dkt.Bashiru,alisema lengo la ziara hiyo limefikiwa kwa kiwango kikubwa kwani ameweza kunadi sera na miongoni ya CCM katika ngazi mbali mbali za chama.

Alieleza kuridhishwa na utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2015-2020 katika mikoa mbali mbali ya Unguja ambayo ni mafanikio yaliyopatikana chini ya Uongozi wa awamu ya saba ya Rais wa Zanzibar DK. Ali Mohamed Shein.

Alisema mafanikio hayo ya ujenzi wa miundombinu ya Barabara,Umeme,Maji,Afya,Elimu na Usafiri wa anga,nchi kavu na majini ni miongoni mwa vielelezo vya ushindi mkubwa utakaopatika mwaka 2020.

Alisema kwa upande wa Zanzibar DK. Shein,amekuwa kiongozi bora aliyefanikisha utekelezaji wa ilani ya CCM ambayo ndio msingi wa ushindi wa Chama katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

Alieleza kuwa Dk. Shein,ameweka mazingira rafiki kwa mrithi wake ajaye kwani atarithi Serikali iliyopiga hatua kubwa kimaendeleo.

Alisema katika ziara hiyo aliwataka viongozi na wanachama kujenga ofisi za kisasa za chama zinazoendana na hadhi ya CCM.

Pia alitoa maelekezo kwa baadhi ya majimbo yenye viongozi ambao ni wabunge na wawakilishi ambao hawafanyi kazi kwa ushirikiano,kuhakikisha kamati za siasa za mikoa husika kusululisha.

Akizungumza baada ya kutembelea vikundi vya Wajasirimali Mkoa huo katika Soko la Mboga Mboga la Mombasa Zanzibar Dkt.Bashiru,alivipongeza vikundi hivyo kwa juhudi zao za kujiajiri wenyewe.

Alieleza kuwa katika kuunga mkono juhudi za Serikali za kutafsiri kwa vitendo Sera ya Mageuzi ya Viwanda nchini ni kuweka Sera,Sheria na mipango endelevu ya kuwawezesha utaalamu na nyenzo wajasiriamali wadogo wadogo ili bidhaa zao ziwe na ubora unaokubalika kitaifa na kimataifa.

“Ujasiriamali ni moja ya njia pekee ya kuwapatia ajira vijana wakajiajiri wenyewe na kupata kipato halali,na hii ndio mipango ya Chama kuitumia vizuri fursa hii kwa maslahi ya wanachama wetu”,alisema Dk.bashiru.

Pamoja na hayo akizungumza wakati wa uwekaji wa mawe ya msingi katika matawi ya CCM katika Mkoa huo,alisema   ngazi za mashina na matawi ndio chimbuko la uimara wa CCM.

Naye Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdulla Juma Mabodi,alisema kuwa CCM inashuka ngazi za matawi,mashina hadi zoni ili kusikiliza changamoto na mafanikio ya Wana CCM na kama zipo changamoto zitatuliwe

Katibu Mkuu huyo leo amekamilisha ziara yake katika Kisiwa cha Unguja na kesho Novemba 2,mwaka 2020 anaendelea ziara yake kisiwani Pemba.