Home Mchanganyiko WAZIRI HASUNGA AWATAKA MAWAZIRI JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI KUDUMISHA MSHIKAMANO

WAZIRI HASUNGA AWATAKA MAWAZIRI JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI KUDUMISHA MSHIKAMANO

0

Sehemmu ya mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakiwa katika mkutano wa 39 wa Baraza la mawaziri la jumuiya ya Afrika Mashariki ulioketi Jijini Arusha tangu tarehe 21-28 Novemba 2019.
Sehemmu ya mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakiwa katika mkutano wa 39 wa Baraza la mawaziri la jumuiya ya Afrika Mashariki ulioketi Jijini Arusha tangu tarehe 21-28 Novemba 2019.
Sehemmu ya mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakiwa katika mkutano wa 39 wa Baraza la mawaziri la jumuiya ya Afrika Mashariki ulioketi Jijini Arusha tangu tarehe 21-28 Novemba 2019.
 
Waziri
wa Kilimo nchini Tanzania Mhe. Japhet Hasunga (Mb) amesema kuwa mawaziri wenzake
wa sekta ya zote ikiwemo sekta ya Kilimo kutoka nchi wanachama wa jumuiya ya
Afrika Mashariki wanapaswa kuendeleza na kuongeza umoja na mshikamano ili kuakisi matakwa ya jumuiya
katika Uzalishaji wa mazao bora ya Kilimo.
Waziri Hasunga
ameyasema hayo tarehe 28 Novemba 2019 wakati akichangia mada kwenye
mkutano wa 39 wa
Baraza la mawaziri la jumuiya ya Afrika Mashariki ulioketi Jijini Arusha tangu tarehe
21-28 Novemba 2019 wa nchi za jumuiya ya Afrika
Mashariki ikiwemo wenyeji Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na Sudani
Kusini.
Mhe
Hasunga alisema kuwa kadri ushirikiano mwema utakavyoendelezwa ikiwa ni pamoja
na kufanya kazi kwa bidii itaimarisha tija na mafanikio ya soko la mazao katika
jumuiya hiyo na dunia kwa ujumla.
Aidha,
amewataka watendaji wote katika nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki kutekeleza
taarifa mbalimbali zinazoandikwa kwa ustadi mkubwa kwani kwa kiasi kikubwa
kumekuwa na utekelezaji duni wa mipango hiyo.
Mkutano huo umefanyika katika ngazi mbalimbali ambapo
Mkutano wa wataalamu ulifanyika tarehe 21-23 Novemba 2019, Mkutano wa makatibu
wakuu ulifanyika tarehe 25-26 Novemba 2019, mkutano wa Mawaziri tarehe 27 -28
Novemba 2019, Kadhalika kutakuwa na Maonesho ya biashara kuanzia tarehe 28-30
Novemba 2019. Aidha mkutano wa wakuu wa nchi uliotarajiwa kufanyika tarehe 30
Novemba 2019 umeahirishwa mpaka mwezi Februari 2020.
Katika
mkutano huo kwa upande wa sekta ya kilimo maswala kadhaa ya sekta ya kilimo
yamejadiliwa na kufikia maazimio Katika kikao cha wataalamu na makatibu wa
wakuu walioazimia kuwa nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki kupitisha
mfumo wa pamoja wa kufanya tathmini ya sekta ya kilimo kwa jumuiya ya afrika
mashariki (Joint Sector Review Mechanism)
Waliazimia
pia kupitisha mfumo wa pamoja wa kufanya uchunguzi wa magonjwa kwa mazao ya mahindi,
mpunga na maharage (Pest Risk Analysis).
Pia wameazimia
pia kuanzisha mahala pa kuzalisha Viuatilifu, na kuwepo kwa miongozo ya
kuhifadhi taarifa za siri za usajili wa Viuatilifu kwa nchi za jumuiya ya
Afrika Mashariki 
Kadhalika,
katika mkutano huo wataalamu walipemdekeza makatibu wakuu kuwashauri
waheshimiwa Mawaziri kuagiza sekretarieti kuwezesha upatikanaji wa rasimu,
mapitio na usainishaji wa makubaliano baina ya nchi mbili au zaidi juu ya
udhibiti wa pamoja wa magonjwa ya wanyama yanayoweza kuvuka mipaka na
kuharakisha utekelezaji wa makubaliano hayo.
Mhe Hasunga ameeleza
kuwa katika mkutano huo pia wamejadili kuhusu kujiunga kwa nchi ya Congo kwenye
jumuiya ya Afrika Mashariki.