Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi,akimpokea Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega,aliyekuwa mgeni rasmi katika kukabidhi chanjo ya mdondo kwa Chama cha Ushirika wa Wafugaji Kuku Bora Jiji la Dodoma (CHAWAKUBODO).
Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega ,akizungumza na wadau kabla hajakabidhi chanjo ya mdondo kwa Chama cha Ushirika wa Wafugaji Kuku Bora Jiji la Dodoma (CHAWAKUBODO).
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi ambaye alimwakilisha mlezi wa CHAWAKUBODO, Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda,akizungumza katika hafla ya kukabidhi chanjo ya mdondo kwa Chama cha Ushirika wa Wafugaji Kuku Bora Jiji la Dodoma (CHAWAKUBODO).
Mwenyekiti wa chama cha wafugaji wa kuku bora Dodoma (CHAWAKUBODO) Bw.Pius Mushi ,akitoa risala kwa mgeni rasmi Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega,wakati wa makabidhiano ya chanjo ya mdondo kwa Chama cha Ushirika wa Wafugaji Kuku Bora Jiji la Dodoma (CHAWAKUBODO)
Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo kutoka wizarani, Dk Makungu Selemani,akizungumza wakati wa makabidhiano ya chanjo ya mdondo kwa Chama cha Ushirika wa Wafugaji Kuku Bora Jiji la Dodoma (CHAWAKUBODO)
Mwenyekiti wa CCM Mtaa wa Mlimwa Kusini Bw.Mohamed Mhando ,akitoa taarifa wakati wa makabidhiano ya chanjo ya mdondo kwa Chama cha Ushirika wa Wafugaji Kuku Bora Jiji la Dodoma (CHAWAKUBODO)
Afisa Mifugo wa jiji la Dodoma ,Gratian Mwesiga ,akisisitiza jambo wakati wa makabidhiano ya chanjo ya mdondo kwa Chama cha Ushirika wa Wafugaji Kuku Bora Jiji la Dodoma (CHAWAKUBODO)
Mkurugenzi wa Utafiti,Mafunzo na Ugani kutoka wizara ya mifugo Dkt.Angello Mwillawa (katikati) akifatilia hotuba ya Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega ,akizungumza na wadau kabla ya kukaabidhi chanjo ya mdondo kwa Chama cha Ushirika wa Wafugaji Kuku Bora Jiji la Dodoma (CHAWAKUBODO).
Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega ,akipokea risala kutoka kwa Mwenyekiti wa chama cha wafugaji wa kuku bora Dodoma (CHAWAKUBODO) Bw.Pius Mushi wakati wa kukaabidhi chanjo ya mdondo kwa Chama cha Ushirika wa Wafugaji Kuku Bora Jiji la Dodoma (CHAWAKUBODO).
Sehemu ya washiriki wakifatilia hotuba ya Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega ,alipokuwa akizungumza na wadau kabla ya kukaabidhi chanjo ya mdondo kwa Chama cha Ushirika wa Wafugaji Kuku Bora Jiji la Dodoma (CHAWAKUBODO)
Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega ,akimkabidhi Mwenyekiti wa chama cha wafugaji wa kuku bora Dodoma (CHAWAKUBODO) Bw.Pius Mushi chanjo ya mdondo kwa Chama cha Ushirika wa Wafugaji Kuku Bora Jiji la Dodoma (CHAWAKUBODO).
Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega ,akisisitiza jambo kwa wanachama wa Chama cha Ushirika wa Wafugaji Kuku Bora Jiji la Dodoma (CHAWAKUBODO) mara baada ya kuwakabidhi chanjo ya mdondo.
Mwenyekiti wa chama cha wafugaji wa kuku bora Dodoma (CHAWAKUBODO) Bw.Pius Mushi,akiwaonyesha wananchama wa Chama cha Ushirika wa Wafugaji Kuku Bora Jiji la Dodoma (CHAWAKUBODO) chanjo ya mdondo.
Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega,akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Chama cha Ushirika wa Wafugaji Kuku Bora Jiji la Dodoma (CHAWAKUBODO) mara baada ya kuwakabidhi chanjo ya mdondo.
……………
Na.Alex Sonna,Dodoma
Serikali imewataka wafugaji na wavuvi nchini kutumia dawati la sekta binafsi lililopo katika wizara Mifugo na Uvuvi ili kuunganishwa na fursa za mikopo na masoko.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega ametoa kauli hiyo leo wakati wa kukabidhi chanjo ya mdondo kwa Chama cha Ushirika wa Wafugaji Kuku Bora Jiji la Dodoma (CHAWAKUBODO).
Amesema kupitia dawati hilo wataongozwa namna ya kuandika andiko mradi ili kupata fursa hizo.
Akizungumzia kuhusu chanjo, Naibu Waziri huyo amesema chanjo anayoitoa imetengenezwa hapa nchini kupitia Taasisi ya Kuzalisha Chanjo (TVI) iliyo chini ya Wizara ambayo imekuwa ikiuza kwa bei nafuu kuanzia Sh.3,500 hadi 4,000 na dozi moja inatosha kuchanja kuku 200.
Ulega amesema mkakati uliopo wa serikali ni kuhakikisha inazalisha chanjo zote muhimu kwa mifugo na kuanza kwa kuzalisha chanjo za magonjwa 11 ya kipaumbele ikiwamo ya magonjwa ya mdondo.
Amewaagiza wataalamu wa ofisi yake kuhakikisha wanawatembelea wafugaji ili kujua changamoto na kuangalia namna ya kuwasaidia.
Naye Mkuu wa Wilaya, Patrobas Katambi ambaye alimwakilisha mlezi wa CHAWAKUBODO, Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda, amewataka wafugaji hao kutumia vyema fursa ya Dodoma kuwa makao makuu kuwa kuwa na mazao yenye ubora.
Naye Mwenyekiti wa CHAWAKUBODO, Pius Mushi amesema chama chao kina wanachama 197 na baada ya mwanachama kununua hisa za Sh. 170,000 anakopesha kuku 500 na chakula cha kutumia kuku kwa mwezi mmoja.
Mushi amesema wanachama wake pamoja na kukabiliwa na changamoto ya magonjwa kwa mifugo yako, ukosefu wa soko la uhakika imekuwa changamoto inayowafanya wafugaji kuwa na woga wa kufuga.
Naye, Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo kutoka wizarani, Dk.Makungu Selemani amesema chanjo iliyotolewa na wizara ambayo ilikuwa ni ahadi ni dozi 100,000 ambayo dozi mmoja ikiuzwa kwa Sh 3,500.