Home Mchanganyiko IGP SIRRO AWATAKA WANANCHI KUTUMIA MADAWATI YA KIJINSIA KURIPOTI UKATILI

IGP SIRRO AWATAKA WANANCHI KUTUMIA MADAWATI YA KIJINSIA KURIPOTI UKATILI

0

*********************************************

27/11/2019 SERENGETI, MARA

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro amewataka wananchi kuacha
kujihusisha na vitendo vya ukiukwaji wa maadili jambo linalopelekea vitendo
vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto.

IGP Sirro amesema hayo leo wakati akizindua Ofisi za dawati la jinsia na watoto
Mugumu wilayani Serengeti mkoani Mara ambapo wananchi wametakiwa
kwenda kuripoti matukio ya ukatili hili hatua ziweze kuchukuliwa.
Aidha, IGP Sirro ameendelea kuwaonya wananchi kuacha mara moja vitendo
vya kihalifu hususani wizi wa mifugo.

Naye Mkurugenzi wa Shirika la Utu wa Mtoto (CDF) bwana Koshuma Mtengete
amesema kuwa, ni vyema jamii ikaendelea kuelimika kwa kutoa taarifa za
unyanyasaji wa kijinsia kwa wanawake na watoto ikiwa ni sambamba na
kutokufumbia macho vitendo hivyo.

Kwa upande Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya ya
Serengeti ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya hiyo Nurdin Babu amesema kuwa,
wilaya yake imeendelea kutoa elimu kwa kuwaelimisha wananchi hususan
kwenye masuala ya kiusalama ikiwemo kuachana na mila kandamizi na
zilizokwisha kupitwa na wakati.