Home Mchanganyiko RAIS WA ZANZIBAR DK ALI MOHAMED SHEIN AZINDUA BOTI MPYA YA KILIMANJARO...

RAIS WA ZANZIBAR DK ALI MOHAMED SHEIN AZINDUA BOTI MPYA YA KILIMANJARO VII ZANZIBAR.

0

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein    akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi na Wafanyakazi wa Boti mpya ya Kilimanjaro VII baada ya kuizindua na kuitembelea iliofanyika katika Hoteli ya Verde mjini Zanzibar.

Mmiliki wa Mradi wa Ujenzi wa Boti Salim Azizi Salim akitoa maelezo kuhusiana na Mtengenezo ya Boti mpya ya Kilimanjaro VII amabayo imezinduliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein katika Hoteli ya Verde mjini Zanzibar.

Waziri wa Fedha na Mipango Baloz Mohamed Ramia Abdiwawa akitoa hotuba ya makaribisho katika hafla ya Uzinduzi wa Boti Mpya ya  Kilimanjaro VII iliofanyika katika Hoteli ya Verde mjini Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein    akibonyeza kitufe cha kulazia Kiti wakati alipotembelea Boti ya Kilimanjaro VII (SABA)Baada ya kuizindua  katika Hoteli ya Verde mjini Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein akisisitiza jambo wakati akitoa hotuba ya Uzinduzi wa Boti Mpya ya Kilimanjaro VII(SABA) hafla iliofanyika Hoteli ya Verde Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein akikata utepe kuashiria Uzinduzi wa Boti mpya ya kilimanjaro VII (SABA)iliofanyika katika Hoteli ya Verde mjini Zanzibar.kushoto ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Baloz Seif Ali Idi,mwengine ni Mwenyekiti wa Makampuni ya Azam Said Salim Bakhresa na kulia ni Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Balozi Mohamed Ramia Abdiwawa.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein akipata maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa Makampuni ya Azam Said Salim Bakhresa kuhusiana na ubora wa Vifaa vya ndani ya Boti mpya ya Kilimanjaro VII(SABA)ikiwemo Viti vya kukunja na kukunjuwa baada ya kuizindua katika Hoteli ya Verde mjini Zanzibar.