Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu amewapongeza Wasanii kwa kuonesha utayari wa kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii katika kunadi vivutio vya Utalii.Kufuatia hali hiyo, Mhe.Kanyasu amewahakikishia Wasanii hao kuwa yeye pamoja na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Hamisi Kigwangala wapo tayari muda wote kutoa ushirikiano kwa Msanii yeyote atakayetaka kufanya kazi na Wizara hiyo.
Akizungumza na wasanii mbalimbali pamoja na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam jana usiku, Mhe.Kanyasu amesema kazi ya sanaa nchini inakua kwa kasi sana, Hivyo wasanii hawawezi kuachwa nyuma katika kutangaza na kuhamasisha Utalii
Katika Mkutano huo uliwakutanisha Wasanii mbalimbali wakiwemo wa wasanii filamu,vichekesho, uchongaji pamoja Washindi wa Miss Utaliu wa miaka minne iliyopita. Mhe.Kanyasu amesema Sanaa ni kichochea cha utalii.
Amesema ushirikiano huo wa Wasanii ni hatua muhimu kwa katika kufikia azma ya Serikali ya awamu ya tano ifikapo mwaka 2020 ni kufikisha idadi ya watalii mbili na nusu.
Akizungumzia mashindano hayo ambayo yanafanyika kwa mara ya nne tangu yalipoanzishwa, Mhe.Kanyasu amewapongeza waandaaji wa Mashindano hayo kwa kubuni vipengele viwili vya kuwatafuta Walimbwende yaani Mlimbwende Utalii wa Tanzania pamoja na Mlimbwende wa Utalii wa Kimataifa. ( Miss Tourism Tanzania & Miss Tourism International )
Amesema ubunifu huo utasaidia kunadi vivutio vya utalii kitaifa kwa kumtumia Mlimbwende wa Utalii wa Tanzania huku vivutio hivyo vya Utalii vitadiwa Kimataifa na Mlimbwende wa Utalii wa Kimataifa.
Ameongeza kuwa mashindano hayo yana sura mpya kwa kuzingatia muono wa Kitaifa na Kimataifa.
Kwa upande wake, Mratibu wa Mashindano hayo, Gideon Chipungahelo amesema vigezo vya kuwapata Washindi hao mbali ya Ulimbwende watakaokuwa nao watazingatia uelewa walionao katika kuvijua vivutio vya Utalii vilivyopo nchini
” Tunamtaka Mlimbwende atakayekuwa balozi wa Utalii na Mwenyekiti ushawishi wa kuwafanya watu wengine wahamasike kutembelea vivutio vya Utalii vilivyopo nchini.” alisisitiza Mratibu huyo..
Akizungumzia maandalizi ya Maonesho hayo, Chipungahelo amesema yataanza mwezi Disemba na kumalizika mwezi Machi mwakani ambapo yatafanyikia jijini Dar es Salaam .
Aidha, Mratibu huyo, Chipungahello amesema kwa upande wa Mashindano ya Utalii wa Kimataifa, nchi 56 zimeonesha utayari wa kushiriki katika Mashindano hayo.
Naye, Mwakilishi wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA,) Anna Masenge amesema Mashindano hayo yatazingatia maadili ya Mtanzani na kamwe hayatakuwa kichocheo cha kuharibu utamaduni huo kwa vile Waandaji hao watazingatia kanuni na miongozo iliyotolewa na BASATA
Kufuatia hali hiyo ametoa wito kwa wazazi kuwaruhusu watoto wao kushiriki katika kinyang’iro hicho huku akiwatoa hofu wazazi kuwa Mashindano hayo sio uhuni kama wengi wanavyoyachukulia.