Home Mchanganyiko RAIS DK.MAGUFULI APOKEA GAWIO LA SH.BILIONI 11 KWA MWAKA 2018 KUTOKA PUMA...

RAIS DK.MAGUFULI APOKEA GAWIO LA SH.BILIONI 11 KWA MWAKA 2018 KUTOKA PUMA ENERGY TANZANIA

0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipokea mfano wa hundi ya gawio yenye thamani ya Bilioni 11 kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Mafuta ya PUMA Energy Tanzania Dkt Selemani Majige (wa pili kushoto) akiwa pamoja na Ofisa Mawasiliano na Mwanasheria wa Kampuni hiyo Goodluck Shirima (kulia). Gawio hilo limekabidhiwa leo Ikulu Chamwino, Jijini Dodoma. Katikati ni Spika wa Bunge, Job Ndugai na kushoto ni Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango.

Godluck Shirima kutoka Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania(wa kwanza kushoto) akifuatilia hotuba ya Rais Dk.John Magufuli wakati wa ghafla ya Taasisi, Mashirika na Kampuni kukabidhi gawio kwa Serikali,ambapo Kampuni ya Puma amekabidhi gawio la Sh.bilioni 11 kwa Rais Magufuli leo Novemba 24,Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma

Rais Dk.John Magufuli akiwa na viongozi mbalimbali wa Taasisi,Mashirika na Kampuni baada ya tukio la kukabidhiwa kwa gawio iliyofanyika leo Novemba 24,Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma

…………………

Na.Alex Sonna,Dodoma

WAKURUGENZI wa Kampuni  ya Puma Energy Tanzania wamependekeza gawio la sh. bilioni 22 kwa mwaka unaoishia Desemba mwaka jana ambapo kila mwanahisa atapata sh. bilioni 11.

Aidha, imesema kuwa mwaka 2017 gawio lilikuwa sh. bilioni 18, 2016 sh. bilioni 14 na mwaka 2015 sh. bilioni 9.

Mkurugenzi Mtendaji wa Puma Energy, Dominic Dhanah aliitoa kauli hiyo leo jijini Dodoma wakati akikabidhi  gawio la Sh.bilioni 11 kwa Rais Dk. John Magufuli Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.

Amebainisha  kuwa ni kuwa kampuni inamilikiwa kwa pamoja na serikali (Kupitia Msajili wa Hazina, Wizara ya Fedha) pamoja na Puma Investments Limited, kila moja ikiwa na umiliki wa hisa kwa asilimia 50.

“Wakurugenzi wa kampuni wamependekeza gawio la Sh.bilioni 22 bolioni kwa mwaka ulioishia Disemba 2018. Hivyo Kila mwanahisa atapata shilingi 11 bilioni. (2017 gawio lilikuwa 18 bilioni, 2016 gawio lilikua 14 bilioni na 2015 gawio lilikua 9 bilioni.)

Amesema  kuwa kutokana na utendaji mzuri wa kampuni ya Puma Energy, gawio limekua kwa asilimia 57 ikilinganishwa na gawio la mwaka 2016 na kwa asilimia 22 ikilinganishwa na gawio na mwaka 2017.

Amefafanua  kuwa ukuaji huu unaendana sambamba na mikakati ya kampuni ya kuhakiksha kampuni inaendelea kukua, kutengeneza faida, kukuza ajira nchini, kuchangia pato la taifa kupitia kodi, na kuendelea kuiunga serekali mkono katika kuwaletea wananchi wa Tanzania maendeleo,”imesema taarifa hiyo

Amesema kuwa  kampuni ya Puma ni ya mkondo wa kati kimataifa katika masula ya mafuta na pia kampuni ya mafuta inayojihusisha na uhifadhi mkubwa na usambazaji.

Ameeleza kuwa  majukumu makuu ya kampuni ni masoko na usambazaji wa bidhaa za petroli ndani ya Tanzania. Kampuni inauwezo wa kuhifadhi jumla ya lita za mafuta milioni 94, vituo 52 vya mafuta maeneo mbalimbali nchini na inahudumia viwanja vinane vya ndege.

Amesema kuwa  kufikia mwisho wa mwaka ulioishia Desemba 31 2018 kampuni ilitengeneza faida kabla ya kodi ya jumla ya Shilingi bilioni 25 na iliwekeza takribani sh. bilioni 16 kwa mwaka 2018 kununua na kuendeleza miundombinu ikiwemo ukamilishwaji wa mfumo wa kujazia mafuta katika jengo namba Tatu (Termina 3) katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Dar e salaam.

Aidha, ununuzi wa vituo viwili vya mafuta kwenye jiji la Dodoma ikiwa ni kuiunga serekali mkono katika kuhamia Dodoma.

Aliweka wazi kuwa ufanisi wa kibiashara wa Puma kwa mwaka 2018 ulikua mzuri kwa pande zote za mauzo pamoja na mapato na unatokana na biashara ya mafuta ya ndege ambako kwa sasa sisi ndio tunaongoza katika soko.

Pia, amesema kuwa taaarifa za masoko zilizochapishwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji(EWURA) inaonesha kuwa uwepo wa Puma Energy kwenye soko la mafuta umeongezeka kutoka asilimia 12 mwaka 2015 hadi asilimia 14 kwa mwaka 2017.

Ameongeza kuwa juhudi za serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Magufuli na Serikali yake katika mikakati yake ya kukusanya kodi, kutoa fursa kwa wawekezaji wa nje na ndani na kuanzisha miradi mikubwa ya kimkakati kama ilivyooneshwa kwenye bajeti ya 2019/20.

Amesema kuwa mikakati hiyo imewezesha kampuni hiyo kupata kazi ya kuuza mafuta katika mradi wa reli ya kati “standa gauge”, mradi wa bwawa la umeme la Mwl. Julias Nyerere kule Rufiji, Daraja jipya la Salender na miradi mingine mingi ya kimkakati.

Amefafanua kuwa miradi hiyo mikubwa inatoa fursa kwa wawekezaji mbali mbali kufanya biashara na kufanya makampuni mengi ikiwemo Puma kutengeneza faida zaidi.

Ameongeza kuwa, Puma itaendelea kufanya kazi kwa ukaribu zaidi na Serikali ya Awamu ya tano, na kuendelea kuchangia katika maendeleo ya taifa, hivyo uongozi wa utaendelea kutoa ushrikiano kama ambavyo wamekua wakishirikiana siku zote.

Naye, Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Mafuta ya Puma Energy, Dk. Selemani Majige amesema kuwa  gawio la sh. bilioni 11 walilotoa linaweza kuwa ni  dogo lakini kwa sasa wanapambana kuhakikisha linaongezeka.

“Lazima tuonyeshe kuwa Puma ni kampuni ya mafuta inayoongoza kwa biashara nchini, tuna vituo maeneo mbalimbali hivyo watanzania watuunge mkono kwenye ununuzi wa mafuta ili kuleta maendeleo,”amesisitiza Dkt.Majige