Home Siasa WAZIRI JAFO ATAHADHARISHA VURUGU KWENYE UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA HAPO KESHO

WAZIRI JAFO ATAHADHARISHA VURUGU KWENYE UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA HAPO KESHO

0

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dodoma wakati akizungumzia kuelekea kwenye upingaji kura Uchaguzi Serikali za Mitaa utakaofanyika kesho nchini kote.

Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo vya habari mbalimbali wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo,wakati akizungumzia  upingaji kura Uchaguzi Serikali za Mitaa utakaofanyika kesho nchini kote.

PICHA NA ALEX SONNA-FULLSHANGWEBLOG

…………………..

Na.Alex Sonna,Dodoma

Kuelekea katika uchaguzi wa serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika hapo kesho, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo, amewataka wananchi kushiriki katika zoezi hilo bila kujihusha na viashiria vya uvunjifu wa amani au kuvuruga uchaguzi huo.

Pia amesema uchaguzi huo utafanyika katika maeneo mbalimbali hapa nchini isipokuwa mikoa mitatu ya Katavi, Ruvuma na Tanga ambapo wagombea wake katika vyama mbalimbali walipita bila kupingwa.

Waziri Jafo ameyasema hayo leo Jijini Dodoma wakati akizungumza na wanahabari kuhusu uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika kesho maeneo mbalimbali hapa nchini, Waziri Jafo amewataka wananchi na wagombea kutojihusisha na vitendo vyovyote vitakavyopelekea kuharibu uchaguzi huo.

” Niwaombe wa Tanzania kwa umoja wao wahakikishe zoezi hilo linafanyika kwa amani na utulivu na kuchagua viongozi watakaowafaa katika maeneo yao, wajiepushe na vitendo vya kupiga Kampeni wakati wa kupiga kula, na ikiwamo kuvaa sare za vyama vyao” amesema Waziri Jafo.

Huku akibainisha kuwa zoezi la uchaguzi litafanyika katika maeneo mbalimbali isipokuwa katika mikoa ya Tanga, Ruvuma na Katavi ambako wagombea wao katika vyama mbalimbali walipita bila kupingwa hivyo zoezi hilo halitawahusu.

Ameongeza kuwa ” zoezi la kupiga kura litaanza saa mbili kamili asubuhi na kumalizika saa kumi kamili jioni na wale wote ambao muda huo utawakuta kwenye foleni wataruhusiwa kupiga kura wakati wale watakaofika baada ya mda huo hawataruhusiwa kupiga kura kabisa” amesema.

Aidha amesisitiza wale wenye mahitaji maalumu kupewa kipaumbele kama vile walemavu, Wazee, wajawazito na wenye watoto wadogo kama desturi ya watanzania waliyozoea siku zote.

Amesema vyama vyote vitakuwa na mawakala ambao watasimamia mazoezi hayo yote kuanzia kupiga kura hadi zoezi la kuhesabu kura ili kila mtu apate haki yake ya kimsingi katika uchaguzi huo, na watahakikisha matokeo ya maeneo yote yatapatikana kesho hiyohiyo.

Amesema vyama vyote kumi na tisa(19)vyenye usajili itashiriki zoezi hilo licha ya kuwa baadhi ya vyama vilitoa matamko ya kujitoa lakini baadhi yao hawakukamilisha matakwa ya kujitoa hasa la kuwa na wadhamini waliowadhamini kwani hawakudhaminiwa na makao makuu ya vyama vyao.

Katika zoezi hilo vyama vyote vitashiriki licha ya kuwa hakuna idadi kamili ya vyamba hivyo, lakini vyote vitashiriki na siku ya Jumanne tathmini halisi ya vyama vingapi vilishiriki itatolewa.