Home Biashara Wadau wakutana kujadili ustawi wa huduma ya pesa kwa njia ya simu...

Wadau wakutana kujadili ustawi wa huduma ya pesa kwa njia ya simu ya mkononi Afrika

0

Mkurugenzi wa M-Pesa Ltd, Epimack Mbeteni akizungumza kwenye kongamano hilo 

Mwakilishi kutoka Benki Kuu ya Tanzania Albert Cesari (wa pili kulia) katika picha ya pamoja na  Mkurugenzi  mkuu wa Vodacom Tanzania Plc, Hisham Hendi (wa kwanza kulia), Mtendaji mkuu, Sheria na Udhibiti kutoka Vodacom Group, Judith Obholzer (wa kwanza kushoto) na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano, Rosalynn Mworia wakati wa kongamano na uzinduzi wa ripoti kuhusu kuhakikisha ukuaji wa huduma za kifedha kupitia simu za mkononi jijini Dar Es Salaam.

Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Plc, Rosalynn Mworia (kulia) na Mtendaji mkuu, Sheria na Udhibiti kutoka Vodacom Group, Judith Obholzer (katikati) wakizungumza na mdau wa huduma za kifedha aliyehudhuria kongamano hilo.

*************************************

Novemba 19, 2019, Dar es Salaam. Wawakilishi kutoka zaidi ya nchi 8 Afrika wanakutana leo katika kongamano maalumu lililoandaliwa na Vodacom kujadili mwenendo na maendeleo kwaajili ya kuboresha sekta ya huduma ya pesa kwa njia ya simu ya mkononi Afrika. Kampuni hiyo inayoongoza kwa teknolojia ya mawasiliano pia imetoa ripoti yake ya kuhakikisha ukuaji wa Huduma
za Kifedha kupitia simu za mkononi katika kongamano hilo.

Ripoti hiyo ambayo ni ya kwanza ya Mwendelezo wa Sera ya Umma kwa Vodacom, inafafanua jinsi ambayo huduma ya pesa kwa simu ya mkononi inayoendesha ukuaji wa uchumi na kuinua kiwango
cha maisha kupitia huduma ya kifedha.

Mkurugenzi Mtendaji, Sheria na Udhibiti wa Vodacom Group, Judith Obholzer, alisema Nchi za Afrika zilizoko Kusini Mwa Jangwa la Sahara ikiwamo Tanzania zimeshuhudia ukuaji wa haraka katika huduma za pesa kupitia simu ya mkononi, sambamba na uvumbuzi na kuwezesha ushiriki mpana wa utoaji wa huduma za kifedha.

Kusini mwa Jangwa la Sahara ni kinara ambapo watu wazima wengi wanamiliki akaunti za simu ya mkononi kuliko zile za taasisi za kifedha. Mabadiliko haya katika ukanda huo yanazidi kuendesha kukua kwa uchumi na faida za kijamii kwa kutoa huduma za kifedha kwa mamilioni ya watu wanaomiliki simu ya mkononi, lakini pia wakiwa umiliki mdogo sana wa akauti za benki.

“Lengo letu ni kutoa jukwaa kwa wataalamu wa sekta hii kutoa maoni yao jinsi ya kuboresha sekta.

Sekta hii inaendelea kukua kwa kasi, watunga sera pamoja na wasimamizi wana jukumu la kuweka mazingira ya biashara hii ya kifedha,” alisema Obholzer.

Mwakilishi kutoka Benki Kuu ya Tanzania ambaye ni Meneja Msaidizi katika idara ya Mifumo ya Malipo ya Taifa, Bwana Albert Cesari alieleza umuhimu wa huduma za kifedha zinazotolewa na makampuni za simu katika utowaji wa fursa pamoja na ajira na ukuwaji wa uchumi.

“ Serikali imeweka mazingira bora na endelevu kuhakikisha huduma za kifedha zinaendelea kuleta mabadiliko chanya ya kiuchumi ikiwemo ajira na mabadiliko katika mfumo wa ulipiaji huduma nchini. Kanuni za malipo ya simu kupitia simu ya mkononi hutolewa ili kuongoza soko bila kuzuia ubunifu au kukwaza mafanikio ambayo yanaletwa na wavumbuzi hawa.”

M-Pesa imekuwa moja ya huduma bora zaidi ya pesa ya simu ya mkononi barani Afrika. Tafiti zinaonesha kwamba huduma ya pesa kupitia simu ya mkononi imechangia kwa kiasi kikubwa katika uwezeshaji wa jamii, kukua kwa uchumi na kupunguza umasikini.

Inatoa huduma kwa njia salama, Uhakika na ya bei nafuu kwa kutuma na kupokea pesa, kuongeza muda wa maongezi, kufanya malipo ya bili, kupokea mishahara na kupata mkopo wa muda mfupi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa utafiti mpya juu ya matumizi ya huduma ya pesa kupitia simu ya mkononi Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Hisham Hendi, alisema “ Huduma ya pesa kwa simu ya mkononi imeongezwa nguvu matumizi ya simu ya mkononi, imeonekana kuwa kama jukwaa la kutoa fursa kiuchumi na kubadlisha mazingira ya huduma za kifedha na hasa katika
bara la Africa,”

Hendi aliongeza kusema kuwa, “Nimefurahi kwamba ripoti hii inaleta pamoja michango ya wataalam wanaoongoza na ndio wazungumzaji katika mada hizi tatu pana. Wana maoni na mitizamo tofauti, ili kuleta msukumo wenye tija na wa kujenga.”

Hafla hiyo iliwashirikisha wawakilishi kutoka kwa waendeshaji wa mitandao ya simu wakiwamo wadau wa mawasiliano, watoa huduma za kifedha, benki, Asasi za Kiraia na washiriki wengine walioshiriki kuchangia mada mbalimbali kama vile; Uthibitisho wa baadaye wa Uwepo wa Huduma za Kifedha za simu ya Mkononi, Mfumo wa Ushirikiano, Mfumo wa Malipo, Ushirikiano wa kikanda
na fursa za mipaka, Jinsi ya kutatua matatizo ya kisheria, Tabia ya kupeana mawazo na fursa za ushindani.