Home Mchanganyiko WIZARA YA KILIMO WAKUTANA NA WADAU WA KILIMO CHA TUMBAKU HAPA NCHINI

WIZARA YA KILIMO WAKUTANA NA WADAU WA KILIMO CHA TUMBAKU HAPA NCHINI

0

Na Ezekiel Mtonyole, Dodoma.

Wizara ya Kilimo imekutana na wadau na wakulima wa kilimo cha Tumbaku hapa nchini ili kujadili changamoto zilizopo katika sekta hiyo nakuzitatua ili kuinua sekta ya kilimo cha Tumbaku hapa nchi.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa kikao hicho kilichofanyika Jijini Dodoma na kuwakutanisha Wizara ya kilimo, fedha na wadau wa kilimo cha Tumbaku, wakulima na makampuni yanayonunua zao la Tumbaku na wenye viwanda vya Tumbaku, naibu Waziri wa Kilimo Husain Bashe.

Amesema lengo la kukutana na wadau hao ni kuhakikisha Wanakutana kwa pamoja na kujadili changamoto na vikwazo vyote vinavyopelekea kutoendelea kwa kilimo cha Tumbaku hapa nchi pamoja na ili kwa pamoja kuona namna ya kuondoka hapa tulipo.

“Tumekutana hapa lengo likiwa ni kuangalia ni namna gani tunaweza kutoka hapa tulipo na kwenda mbele, ndio maana tumeshirikisha wadau wote sisi Wizara ya kilimo, fedha, wadau wa kilimo,wenye viwanda na wakulima ili kila mtu ajue nani ni kikwazo na kuanguka kwa sekta hii”

Ameongeza kuwa” zao la Tumbaku uzalishaji wake umekuwa ukishuka siku baada ya siku ukiangalia uzalishaji umeshuka kwa asilimia kubwa toka uzalishaji wa tani laki mojana ishirini (120,000) Hadi kufikia tani arobaini (40) kwa Sasa” amesema Mhe. Bashe.

Amesema katika kikao hicho wameunda kamati ndogo ambayo itapitia sekta nzima ya kilimo cha Tumbaku na kukutana na wadau wote wa kilimo cha tumbaku na kuja na mapendekezo ya pamoja nini kitanyike na Kodi zipi zipunguzwe kwa Afya ya kilimo cha Tumbaku hapa nchini.

Amesema wameamua kuja na vikao hivyo vya kila kila zao peke yake ili kuona kila zao na tatizo lake kwa matatizo mengi yanatofautiana kwa kila zao na hivyo wameona ni vyema kukaa na wadau wa kila zao kuona namna ya kutatua changamoto za kila zao.

Amesema moja ya changamoto zilizoibuka ni baadhi ya makampuni ya ununuzi wa zao la Tumbaku kutaka kujitoa, na wamejadili na makampuni hayo likiwamo kampuni ya TLTC kutokana na kutorudi kwa VAT return lakini baada ya mazungumzo wamekubali kuendelea na ununuzi wa zao hilo.

Amesema lengo kubwa la serikali ni kuona kilimo cha Tumbaku kinaanza kurudi katika uzalishaji wake wa kawaida na kuleta tija kwa serikali na wakulima kunufaika na kazi wanazozifanya.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme, ambaye ni mdau wa kilimo cha Tumbaku amesema ni muhimu kwa taasisi za Serikali kujenga mazingira mazuri kwa wakulima na wafanya biashara wa zao la Tumbaku ili kuondoa migongano ambayo imekuwa ikitokea Mara kwa Mara.

Amesema kwa pamoja kama wakulima ni lazima lazima wasimamie ushirika katika zao hilo ili iwe rahisi katika hata katika kupanga bei, pia amesisitiza wale wanaopanga ubora wa tumbaku kuwa waaminifu na wazalendo kwa kupanga kwa usahihi.

Naye mmoja wa wakulima ambaye pia ni mwanachama wa chama Cha msingi Tabora, Uyui, Said Shabani, mbali na kumpongeza Naibu Waziri wa Kilimo kwa kuwakutanisha, amesema kwa kikao hicho ameanza kuona mwanga katika sekta ya kilimo na Sasa anaamini uzalishaji utaanza kupanda sasa.