Home Mchanganyiko TANZANIA NA ANGOLA KUSHIRIKIANA KATIKA ENEO LA MAFUTA, GESI NA MAPAMBANO DHIDI...

TANZANIA NA ANGOLA KUSHIRIKIANA KATIKA ENEO LA MAFUTA, GESI NA MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA

0

************************************

Na Mwandishi Maalum Dodoma Nov: 15/2019

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Profesa Adelardusi Kilangi, jana
( alhamisi) amekutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi wa
Serikali ya Angola hapa Nchini, Mhe. Balozi Sandro Renato
Agostinho de OLIVEIRA.

Mazungumzo baina ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Profesa
Kilangi na Balozi Sandro Renato Agostinho de OLIVEIRA ambayo
yamefanyika katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali
Jijini Dodoma, yalijikita katika kuangaliana namna gani Ofisi
ya Mwanasheria Mkuu wa Tanzania itakavyoshirikiana na Ofisi
ya Mwanasheria Mkuu wa Angola.

Balozi wa Angola Mhe. Sandro Renato Agostinho de OLIVEIRA,
alimweleza Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Profesa Adelardus
Kilangi kwamba, Serikali yake, yaani Ofisi ya Mwanasheria
Mkuu wa Serikali ingependa kushirikiana karibu na Ofisi ya
Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Tanzania katika maeneo kadhaa
likiwamo namna ya kukabiliana na tatizo la rushwa.

"Tungependa (Angola) kuanzisha mahusiano na masharikiano baina
ya Ofisi yako na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Angola.
Tunaamini kuna maeneo mengi ambayo tunaweza kubadilishana
uzoefu likiwamo hili la kukabiliana na changamoto za
rushwa". Akasema Balozi de OLIVEIRA.

Aidha Balozi huyo wa Angola alisema amefurahi sana kufika
Jijini Dodoma kwa kuwa ilikuwa ni mara yake ya kwanza.
Kwa upande wake Profesa Adelarus Kilangi pamoja na kushukuru
kwa Balozi huyo wa Angola kumtembelea, alimweleza kwamba
Ofisi yake ipo tayari kuanzisha mahusiano na mashirikiano na
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Angola.

AG Kilangi pamoja na kukubaliana kushirikiana na kubadilisha
uzoefu katika eneo la kukabiliana na rushwa, yeye alitaka
ushirikiano pia katika eneo la mafuta na gesi na pia katika
maeneo ya kujengeana uwezo na maarifa katika maeneo
mbalimbali.

Itakumbukwa kwamba, Nchi ya Angola ni kati ya nchi chache za
Bara la Afrika kusini mwa Jangwa la Sahara ambazo zinautajiri
mkubwa wa mafuta na gasi na wanauzoefu wa kutosha eneo
hilo.