Naibu Waziri wa Kilimo, Husain Bashe kulia Akizungumza wakati wa kikao na wadau na wakulima wa Chai hapa nchini walipokutana kujadili changamoto zilizopo katika kilimo cha chai hapa nchini na kuona namna ya kuinua kilimo hicho hapa nchini, kikio kilichofanyika Jijini Dodoma.
Spika Msitaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bi. Anna Makonda, kushoto, akizungumza wakati wa kikao na wadau na wakulima wa Chai hapa nchini walipokutana kujadili changamoto zilizopo katika kilimo cha chai hapa nchini na kuona namna ya kuinua kilimo hicho hapa nchini, kikio kilichofanyika Jijini Dodoma.
Mbunge wa Jimbo la Njombe Mjini(CCM)Edward Mwalongo, Akizungumza wakati wa kikao na wadau na wakulima wa Chai hapa nchini walipokutana kujadili changamoto zilizopo katika kilimo cha chai hapa nchini na kuona namna ya kuinua kilimo hicho hapa nchini, kikio kilichofanyika Jijini Dodoma.
Mbunge na ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya bajeti, Mashimba Ndaki, aliyesimama, akizungumza wakati wa kikao na wadau na wakulima wa Chai hapa nchini walipokutana kujadili changamoto zilizopo katika kilimo cha chai hapa nchini na kuona namna ya kuinua kilimo hicho hapa nchini, kikio kilichofanyika Jijini Dodoma.
Baadhi ya wadau wa kilimo waliohudhuria kikao na wadau na wakulima wa Chai hapa nchini walipokutana Jijini Dodoma kujadili changamoto zilizopo katika kilimo cha chai hapa nchini na kuona namna ya kuinua kilimo hicho hapa nchini, kikio kilichofanyika Jijini Dodoma.
………………..
Na Ezekiel Mtonyole, Dodoma.
Wizara ya kilimo imekutana na wadau na wakulima wa chai hapa nchini kujadili namna ya kulitoa zao hilo hapo lilipo na kwenda sehemu nyingine ili liweze kuleta tija kwa wakulima na kuongeza Pato la taifa.
Akizungumza Mara baada ya kikao hicho kilichoshirikisha Wizara ya kilimo, fedha, wadau wa kilimo cha chai, wakulima wakubwa na wadogo na Wakurugenzi wa Halmashauri ambako Kuna wakulima wa chai.
Naibu Waziri Bashe amesema lengo lilikuwa ni kuhakikisha Wanakutana na wadau hao kwa pamoja kujadili namna ya kutatua changamoto zinazopelekea kuangushwa sekta ya kilimo cha chai ili kwa pamoja kuongea lugha moja kuhakikisha sekta hiyo inatoka hapo ili kuleta tija.
“Tumekutana na wadau hawa kutoka sehemu mbalimbali ikiwamo Wizara ya fedha ili kuona ni namna gani tunaweza kuliinua kwa kuondoa changamoto zilizopo katika sekta hiyo” amesema Mhe. Bashe.
Amesema kwa pamoja wamejadili kuhusu sekta ya chai zinazoikabili sekta ya hiyo kwanini kwa miaka mingi sekta ya kilimo cha chai kwani kwa miaka kumi (10) sekta hiyo imekuwa kwa asilimia 1 tu hivyo juhudi za pamoja zinatakiwa kuokoa zao hilo.
Ameongeza kuwa ” imeundwa timu inayoshirikisha sekta binafsi na Serikali na taasisi zinazosimamia chai na wametengeneza mpango mkakati wa miaka mitano (5) ambayo itasimamia kwenda mbele kwa sekta ya kilimo cha chai, ili itoke kwenye uzalishaji wa tani elfu 37, Hadi kufikia tani laki moja” amesema.
Amesema wakati wa kujadili changamoto limeibuka suala la VAT return na wamekubaliana na Kamishna Mkuu wa mamlaka ya mapato Tanzania, TRA, kukutana siku ya juma nne kujadili suala hilo na kukutana na viwanda vyote vya chai hapa nchini kujadili suala hilo.
Changamoto nyingine waliyojadili ni ya wasafilishaji ya kutokuwa na sehemu ya pamoja ya kukusanyia mazao yao, na wanaandaa makontena zote zikufanywe sehemu moja na kuandaliwa vibali kwa pamoja, pia wanaandaa mpango wa kuanzisha kwa mnada wa zao la chai Dar es saalam.
Pia amesema wameona Kuna haja ya kufanyia mabadiliko baadhi ya Sheria, na wataanza kulifanyia kazi katika mwaka wa fedha ujao, pia kumekuwa na suala la watu kutolipwa kwa wakati na ameagiza wakulima walipwe ndani ya siku 15 kwa mujibu wa Sheria na taratibu.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa usimamizi bodi ya Chai Tanzania, Kemerina Kafanabo, amesema kupitia kikao hicho pia wameangalia suala la ubovu wa miondombinu ambayo imekuwa chanzo Cha kuharibika kwa chai kabla ya kufika kiwandani toka shambani.
Pia wamezungumzia ubora wa chai sambamba na kuongeza upatikanaji wa pembejeo ili kuongeza ubora wa chai, pia wameiomba serikali kuongeza wataalamu wa kilimo maeneo hayo ili kuongeza ubora wa chai inayozalishwa kwenye viwanda hivyo, pamoja na kuongeza vitendea kazi