
Na Silvia Mchuruza,Bukoba
Watu wenye ulemavu watakiwa kujitokeza kushiriki katika uchaguzi ikiwa watu 13 kati ya 19 wamefanikiwa kuteuliwa katika kugombea nafasi za uenyekiti Wa serikali za mtaa katika uchaguzi utakaofanyia tarehe 24 Nov.mwaka huu mkoani kagera.
Akizungumza katibu Wa chama cha walemavu mkoani kagera SHIVYAWATA Bw. Swertbert Mshanga amesema kuwa ushiriki wao katika mchakato Wa uchaguzi utawafanya kuwatia moyo walioteulia kugombea katika uchaguzi huku watu watu 13 walibahatika kupita lakini pia ameongeza na kusema kuwa idadi hiyo bado ni ndogo katika mkoa.
Hata hivyo amesema kuwa bado viongozi Wa vyama awajatambua uwezo Wa watu wenye ulemavu katika uongozi ikiwa ni changamoto kubwa na kuperekea wanachama walio wengi kubweteka na kutokuwa na kadi huku akiitaka serikali kutoa hama kwa watu wasio walemavu kuelewa kuwa na wak nanaweza.
Aidha amesama kuwa watu wenye ulemavu awana utetezi Wa kutosha kutokana na kutokubaliwa kwa asilimi mia moja katika jamii inayowazunguka na kuiomba serikali kutambua mchango wao katika uongozi pia ametoa wito kwa jamii kuwataza watu wenye ulemavu kwa sura tofauti na kuamini kuwa wana uwezo Wa kuongoza katika serikali.
Samba na hayo amewataka hata watu wenye ulemavu kutojinyanyapaa kutokana na hali iliyopo katika jamii licha ya jamii kutoitambua zaidi nafasi waliyo nayo katika ngazi mbali mbali za uongozi.