**************************************
Na Shushu Joel
MAMLAKA ya mapato Tanzania (TRA) imewataka wananchi kujenga utamaduni wa kuchukua risiti kwa kila manunuzi wanayofanya kwa kuwa kutokuchukua risiti ni kosa kisheria.
Akizungumza na baadhi ya wateja katika moja ya vituo vya mafuta vilivyoko wilaya ya Kibiti mkoani Pwani Mkurugenzi wa huduma ya elimu kwa walipa Kodi Richard Kayombo alisema kuwa wananchi walio wengi hawachukui risti zao mara baada ya kuhudumiwa.
Alisema kuwa kitendo wanachokifanya ni hasara kwao kwani inaweza imatokea kitu kibaya katika biashara hiyo huku risti uliacha kwenye kituo cha mafuta hivyo msaada wako utakuwa ni mdogo sana ukilinhanisha na ukiwa na risti.
“Nasikitika sana kuona kuna ndoo iliyojaa risti zilizoachwa na watu ambao wamwhudumiwa mafuta,jamani risti ni muhimu sana pia ni kosa kisheria kutokuchukua risti yako”Alisema Kayombo.
Kayombo amesema kuwa Sheria ya usimamizi wa Kodi inatanabaisha kuwa mtu yoyote asiyechukua risiti anafanya kosa kisheria na anaweza kutozwa faini kuanzia shilingi 30,000 hadi 1.5ml au kwenda jela kifungo kisichozidi mwaka mmoja.
“Sheria iko wazi kabisa lakini TRA tunawasisitiza wateja wote kudai na kuchukua risiti kila wanaponunua bidhaa au kupata huduma”, amesema.
Aidha aliongeza kuwa mamlaka ya mapatoTanzania imeanzisha mfumo wa utoaji wa elimu kwa mikoa miwili miwili ingawa kwa sasa tumwanza na mkoa wa Morogoro na Pwani kisha baada ya hapo tutaenda mikoa mingine miwili kwa lengo la kuwaelimisha wananchi.
Mbali na hilo Kayombo amewasisitiza wananchi wote kulipa kodi ya majengo mapema ili kuondoa usumbufu wa mwisho wa mwaka kama walivyozoea.
“Wananchi wwngi wamekuwa wakishindwa kuelewa ni kwanini wanasisitizwa kulipa kodi, jamani Kodi ndio zinaleta maendeleo nchini hivyo mkilipa kwa uaminifu maendeleo makubwa mtayaona “Alisema.
Pia amempongeza Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kupeleka maendeleo makubwa sehemu m alimbali kwa kusudi la wananchi kutambua thamani ya Kodi zao wanazolipa.
Naye Juma Ally mkazi wa kibiti amewapongeza TRaA kwa kujitoa kwa wananchi katika kuwaelisha juu ya masuala ya kulipa kodi .
Aliongeza kuwa wananchi mnapaswa mjitokeze kwa wingi ili muweze kuvuna elimu hii maana ni ya muhimu sana kutambua kiwango chako cha ulipaji Kodi.
Kwa upande wake Fatma Hamadi ni mmoja wa wafanyabiashara wa duka katika wilaya ya Kibiti ameipongeza serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt Magufuli kwa usimamizi wake wa miradi kwa kutuonyesha wananchi kile tunachokitoa kupitia Tra kukiona kialisia kweli huyu ni mtetezi wetu.
Aidha amiopongeza mamlaka ya mapato nchini TRA kwa elimu wanayoitoa kwa jamii.